Wanawake Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar,
wanakabiliwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyofanywa na maafisa
usalama katika vituo vya polisi nchini humo. Kwa mujibu wa ripoti
maafisa wa usalama nchini Myanmar wamekuwa wakiwateka nyara wanawake na
wasichana Waislamu wa kabila hilo sanjari na kuwapiga na kuwatukana.
Habari zinasema kuwa, baada ya maafisa hao kuwalazimisha kutumia madawa
ya kulevya huwapeleka katika vituo vya usalama na kuwabaka bila ya wao
kujielewa. Hii ni katika hali ambayo jamii ndogo ya Waislamu nchini humo
imekuwa ikinyimwa haki zake za kimsingi kutokana na serikali ya
Naypyidaw kupinga kuwapa Waislamu wa jamii hiyo haki yoyote kwa madai
kuwa eti sio raia wa nchi hiyo. Aidha kwa mara kadhaa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa ya kutetea haki za binaadamu yamekuwa yakiituhumu serikali
ya nchi hiyo kwa kufumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia
vimavyofanywa na maafisa wa usalama na jeshi dhidi ya wanawake Waislamu
wa kabila la Rohingya nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment