Rais Mahamadou Issoufou wa Niger ametahadharisha uwezekano wa
Libya kutumbukia kwenye machafuko makubwa zaidi kama ilivyowahi kuikumba
Somalia. Akizungumza pambizoni mwa kikao cha usalama na amani barani
Afrika huko Paris nchini Ufaransa, Rais Issoufou ameongeza kuwa, hali
ya Libya ni tete mno kwani harakati za makundi ya kigaidi na wanamgambo
wa Kisalafi zinazidi kuongezeka na kuuawa makumi ya watu kila uchao
katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Rais wa Niger amesisitiza
udharura wa kurejeshwa amani na utulivu nchini humo. Niger ambayo
inapakana na Libya upande wa kusini, imekuwa ikikabiliana na makundi
yenye kuchupa mipaka ndani ya ardhi ya Niger ikisaidiana na washirika
wake wa Magharibi na nchi majirani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment