Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, December 30, 2013

Hofu ya UN kuhusu hali ya wakimbizi S/Kusini


Hofu ya UN kuhusu hali ya wakimbizi S/KusiniUmoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusu idadi inayoongezeka ya watu wanaokimbia makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea huko Sudan Kusini kati ya jeshi la serikali ya Juba na waasi wanaoongozwa na makamu wa zamani wa rais wa nchi hiyo Riek Machar.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) ulitangaza jana kuwa karibu watu laki moja na 80 elfu wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano ya ndani yanayoendelea katika nchi hiyo change zaidi duniani. Taarifa ya ujumbe huo imesema wakimbizi 75 elfu wamepewa hifadhi katika kambi za Umoja wa Mataifa katika maeneo ya Juba, Bor, Bentiu na Pariang tangu mapigano hayo yaanze katikati ya mwezi huu wa Disemba.
Wakati huo huo jumuiya za misaada ya kibinadamu zimetahadharisha kuwa maelfu ya watoto wadogo wametenganishwa na wazazi wao kutokana na machafuko ya Sudan Kusini.
Mapema jana Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa wapiganaji wa Riek Machar wanakaribia makao makuu ya jimbo la mashariki la Jonglei na kwamba mapigano makali yameshuhudiwa kati ya pande mbili hasimu katika njia ya kuelekea Bor.

No comments:

Post a Comment