Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, December 30, 2013

Watu 15 wauawa katika mlipuko wa basi Russia


Watu 15 wauawa katika mlipuko wa basi Russia
Watu wasiopungua 15 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea ndani ya basi la abiria mapema leo katika mji wa Volgograd huko kusini mwa Russia.
Mlipuko huo umetokea wakati basi hilo lilipokuwa linakaribia soko la mji huo la umeharibu viyoo vya nyumba jirani.
Naibu Gavana wa mji wa Volgograd, Vasily Galushkin amesema ripoti alizonazo zinasema kuwa watu 15 wameuawa katika mlipuko huo na makumi ya wengine kujeruhiwa. Wataalamu wa serikali ya Russia wanasema kuwa mlipuko huo umetokana na shambulizi la kigaidi.
Shambulizi hilo limetokea siku moja tu baada ya hujuma nyingine ya bomu katika kituo kikuu cha treni cha mji wa Volgograd ambayo imesababisha vifo vya watu 17 na kujeruhi wengine wengi.
Hadi sasa hakuna mtu au kundi lililodai kuhusika na mashambulizi hayo ambayo yamefanyika kabla ya michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi ya Sochi iliyopangwa kufanyika mwezi Fubruari mwakani.

Wanawake Waislamu Myanmar wabakwa na polisi



Wanawake Waislamu Myanmar wabakwa na polisi
Wanawake Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar, wanakabiliwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyofanywa na maafisa usalama katika vituo vya polisi nchini humo. Kwa mujibu wa ripoti maafisa wa usalama nchini Myanmar wamekuwa wakiwateka nyara wanawake na wasichana Waislamu wa kabila hilo sanjari na kuwapiga na kuwatukana. Habari zinasema kuwa, baada ya maafisa hao kuwalazimisha kutumia madawa ya kulevya huwapeleka katika vituo vya usalama na kuwabaka bila ya wao kujielewa. Hii ni katika hali ambayo jamii ndogo ya Waislamu nchini humo imekuwa ikinyimwa haki zake za kimsingi kutokana na serikali ya Naypyidaw kupinga kuwapa Waislamu wa jamii hiyo haki yoyote kwa madai kuwa eti sio raia wa nchi hiyo. Aidha kwa mara kadhaa Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kutetea haki za binaadamu yamekuwa yakiituhumu serikali ya nchi hiyo kwa kufumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia vimavyofanywa na maafisa wa usalama na jeshi dhidi ya wanawake Waislamu wa kabila la Rohingya nchini humo.

Maandamano yaendelea Misri, makumi wajeruhiwa


Maandamano yaendelea Misri, makumi wajeruhiwa
Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Misri wameendelea kuandamana leo wakipinga ukandamizaji uliofanywa na vyombo vya usalama dhidi ya wanafunzi wenzao wa Chuo Kikuu cha al Azhar mjini Cairo katika siku chache zilizopita.
Maandamano haya yanafanyika huku idadi ya watu waliojeruhiwa katika machafuko ya jana mjini Cairo ikiendelea kuongezeka. Idadi kubwa ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha al Azhar walijeruhiwa baada ya askari usalama wa serikali ya mpito ya Misri kushambulia uwanja wa chuo hicho na kutawanya wanafunzi waliokuwa wakiandamana kupinga mapinduzi ya kijeshi yaliyoiondoa madarakani serikali ya Muhammad Mursi.
Jeshi la Misri limewakamata wanafunzi kadhaa wa Kitengo cha Biashara cha Chuo Kikuu cha al Azhar siku moja baada ya polisi kuua mwanafunzi mmoja na kujeruhi wengine kadhaa katika jaribio la kutawala maandamanao ya wanafunzi wanaopinga utawala unaoungwa mkono na jeshi la Misri.

Hofu ya UN kuhusu hali ya wakimbizi S/Kusini


Hofu ya UN kuhusu hali ya wakimbizi S/KusiniUmoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusu idadi inayoongezeka ya watu wanaokimbia makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea huko Sudan Kusini kati ya jeshi la serikali ya Juba na waasi wanaoongozwa na makamu wa zamani wa rais wa nchi hiyo Riek Machar.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) ulitangaza jana kuwa karibu watu laki moja na 80 elfu wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano ya ndani yanayoendelea katika nchi hiyo change zaidi duniani. Taarifa ya ujumbe huo imesema wakimbizi 75 elfu wamepewa hifadhi katika kambi za Umoja wa Mataifa katika maeneo ya Juba, Bor, Bentiu na Pariang tangu mapigano hayo yaanze katikati ya mwezi huu wa Disemba.
Wakati huo huo jumuiya za misaada ya kibinadamu zimetahadharisha kuwa maelfu ya watoto wadogo wametenganishwa na wazazi wao kutokana na machafuko ya Sudan Kusini.
Mapema jana Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa wapiganaji wa Riek Machar wanakaribia makao makuu ya jimbo la mashariki la Jonglei na kwamba mapigano makali yameshuhudiwa kati ya pande mbili hasimu katika njia ya kuelekea Bor.

UN yawasaidia waasi wa zamani wa M23 Congo


UN yawasaidia waasi wa zamani wa M23 Congo
Umoja wa Mataifa umewapelekea misaada ya kibinadamu waasi wa zamani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa waliko mashariki mwa nchi hiyo wamepeleka misaada ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na chakula kwa waasi wa zamani wa Kongo wa kundi la M23 wanaohifadhiwa katika eneo lililoko umbali wa kilomita 40 kutoka mji wa Goma katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Jenerali Tim Mukunto wa jeshi la Kongo amesema karibu tani 10 za chakula zinazotosha kwa ajili ya kipindi cha wiki mbili zimekabidhiwa kwa waasi hao wa zamani.
Awali askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na taasisi mbalimbali za kimataifa zilielezea wasiwasi wao kuhusu hali mbaya ya waasi wa zamani wa kundi la M23 nchini Kongo.
Kundi hilo la waasi wa zamani lililazimika kutia saini makubaliano ya amani na serikali ya Kinshasa baada ya kupata kipigo kikubwa katika operesheni ya kijeshi iliyoshirikisha jeshi la Kongo na askari wa kimaraifa.

Saturday, December 21, 2013

Misri yamuondolea Shafiq marufuku ya kusafiri


Misri yamuondolea Shafiq marufuku ya kusafiri
Maafisa nchini Misri wamemuondolea Ahmad Shafiq marufuku ya kusafiri nje ya nchi. Shafiq alikuwa waziri mkuu wa mwisho wa Hosni Mubarak dikteta aliyeng’olewa madarakani katika mapinduzi ya wananchi huko Misri.  Mamlaka inayohusika na hati za kusafiria ya Misri imewaagiza maafisa wa uwanja wa ndege kuliondoa jina la Jenerali Ahmad Shafiq katika orodha ya watu wasioruhusiwa kusafiri nje baada ya kutopatikana na hatia katika kesi ya ardhi ya marubani.
Hayo yemeelezwa na duru moja ya kiwanjani hapo ambayo haikutaja jina lake. Kuondolewa kwa marufuku hiyo ya kusafiri kumejiri baada ya mahakama moja ya Misri kuwafutia mashtaka ya ubadhirifu tarehe 19 mwezi huu, waziri mkuu huyo wa zamani na pia watoto wawili wa dikteta Hosni Mubarak  yaani Alaa na Gamal.
Ahmad Shafiq alikuwa anakabiliwa na mashtakiwa ya kuwauzia ardhi ya serikali kinyume cha sheria watoto hao wawili wa dikteta Mubarak tena kwa bei ya chini kabisa.  

KAMPALA YAPITISHA MSWADA WA KUPINGA NDOA ZA JINSI MOJA



kampala

bunge la uganda limepitisha muswada wa sheria wa kupambana na ndoa za watu wa jinsia moja, ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo mhalifu atakayepatikana na hatia atahukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

muswada huo wa ndoa za watu jinsia moja ulipitishwa na wabunge hapo jana. taarifa zinasema kuwa, wananchi wa uganda wanamsubiri rais yoweri museveni wa nchi hiyo aidhinishe muswada huo wa bunge na kuwa sheria.

muswada huo pia unaeleza kuwa, mtu yeyote aliyekuwa na taarifa za watu wanaoshiriki ngono za watu wa jinsia moja na kushindwa kutoa taarifa hizo kwenye vyombo husika atafungwa jela maisha.

mjadala wa kuchukuliwa adhabu kali watu wanaojihusisha na ngono za jinsia moja, uliibuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2009, lakini madola ya magharibi yaliishinikiza sana uganda, ikalazimisha kusitisha kufuatilia muswada huo.

madola ya magharibi yalitishia kusimamisha misaada yao kwa uganda kama muswada huo ungelipitishwa bungeni.

wabunge walipendekeza itumike adhabu ya kifo kwa mtu yeyote atakayepatikana kwa mara ya pili na hatia ya kujihusisha na ngono za watu wa jinsia moja au kumuambukiza mwenza wake kwa makusudi virusi vya hiv.

SHEIKH ABDULLAH SALEH AL-FARSY (FEBRUARY 12, 1912-NOVEMBER 9, 1982) THE GREAT POET, SCHOLAR AND HISTORIAN IN ZANZIBAR


 
By Khatib Rajab
  When Sheikh Abdullah Saleh al-Farsy (1912-1982) died on November 9, 1982, he was undisputedly one among the international poets, scholars and Muslim historians in Zanzibar. He is remembered with ever smiling face and pleasant manners. He never failed to be surrounded by people who wanted to greet him or discuss about Islam. His reputation extended as far as to Southern Somalia in the north and Cape Town to the south as well as Nyasaland (Malawi), where he conducted DARSA (Lessons) before he left to Kenya to avoid persecution in Zanzibar. Born in Zanzibar on February 12, 1912 to a well distinguished family, Sheikh Abdullah Saleh Farsy studied the Qur'an from Fatma Hamid Said (1854-1936), a student of Sheikh Amin bin Ahmed who taught Qur'an at Jongeani village, where Sheikh Abdullah Farsy was born and raised.
Sheikh Abdullah Saleh Farsy memorised the Qur'an and large portions of Ahadith at a very young age. His strong desire for Islamic and secular education was insatiable and while other people of his age engaged in leisurely activities, Sheikh Abdullah Saleh Farsy was almost always seen deeply engrossed over a new Islamic book. He loved reading so much so that most of his life was engaged in his huge home library.
When Sheikh Abdullah Saleh al-Farsy died, he was the most accomplished and respected ulama in the Swahili-Islamic World. His incomparable contribution to Islam reached its peak with the publication of his 807-page QUR'AN TAKATIFU (Glorious Qur'an), the first accepted complete translation into Swahili.
This enthusiastic and brilliant young scholar was lucky because at that time, Zanzibar retained some of the centuries old Islamic educational institutions. They were filled with students under the guidance of intellectual ulama such as Sheikh Abu Bakr bin Abdullah bin Bakathir (1881-1943), a renowned student of Sayyid Ahmed bin Abu Bakr al-Sumait (1961-1925) whom Sheikh Abdullah Saleh considered him as the greatest Islamic scholar East (and Central) Africa has ever produced.
In 1922, Sheikh Abdullah Saleh Farsy enrolled the BARZA MOSQUE after two ULAMA (Scholars) asked him to do so. First, was Sayyid Hamid bin Mansab (1902-1965) who taught him RISALATUL JAMI'A, an elementary Islamic Studies. This IMAM (Leader) of FORODHANI MOSQUE died during the DARSA at the GOFU MOSQUE. He was a student of Sheikh Muhammad Abdul Rahman Makhzymy (1877-1946), one among the teachers of Abdullah Saleh Farsy. Second, was Sayyid Alawy bin Abdul Wahab (1902-1960) who taught him 12 books on FIQH, Arabic and commentary of MARDFIN RABBIYYAH about inheritance.
Besides mastering the rudimentary teaching of Islam at the BARZA MOSQUE, Sheikh Abdullah Saleh Farsy excelled in Arabic grammar. In his 20s, he was writing Arabic poems, indicating the high level of education that the Zanzibar ulama were capable of disseminating at the time.
Sheikh Abdullah Saleh Farsy studied under the tutelage of many great ulama such as Sheikh Ahmed bin Muhammad al-Mlomry (1873-1936) who taught him 25 books, including the TAFSIR (Exegesis) known as the JALALAYN, after Jalal al-Din Mahali (1389-1450) and Jalal al-Din Suyut (1445-1505), eminent Shafi'i ulama of Syria and Egypt, respectively.
When Sheikh Abdullah Saleh Farsy completed all his instruction at the BARZA MOSQUE, Sheikh Ahmed bin Muhammad al-Mlomry allowed him to teach at the BARZA MOSQUE during Ramadhan under his supervision, analogous to an internship in our modern parlance.
He studied from Sheikh Abu Bakr (1881-1943), the son of Sheikh Abdullah bin Abu Bakr Bakathir (1860-1925), a student of Sheikh Ahmed bin Abu Bakr al-Sumait. Sheikh Abu Bakr bin Abdullah bin Bakathir who taught him more Fiqh than other ULAMA in Zanzibar, attended the DARSA of Sheikh Abdullah Saleh Farsi to give him incentive. He appointed him the IMAM for WITRI from 1933 until October 28, 1939, when he also allowed him the Qur'an reciter in the GOFU MOSQUE and led the FAJR prayers until 1966, when he was replaced by his sister's son Saleh bin Salim bin Zagar.
Sheikh Abdullah Saleh Farsy studied from Sheikh Muhammad Abdul Rahman al-Makhzymy many volumes of FIQH (Jurisprudence), including FUTH AL-MUIN and IKNAI, which was first taught by Sheikh Abdullah bin Abu Bakr bin Bakathir in 1917 at the GOFU MOSQUE. He also taught him the science of determining the proper hours of worshipping and direction of the QIBLA. Although Sheikh Abdullah Saleh first studied MINHAJ AT-TABIN by the GREAT Shafi'i ULAMA Sheikh Zakariya Muhyddin Yahya Sharaff ad-Din al-Nawawi (1213-1277), he then studied it from Sheikh Muhammad Abdul Rahman al-Makhzymy.
The canonical standing of this book in Zanzibar goes back to Imam Abu Hamid bin Muhammad al-Ghazzali (1058-1111), professor of Nidhamiyyah Shafi'i Muslim Academy in Baghdad. He was a student of Imam of HARAMAYN Ahmed Malik al-Jawayti (d. 1085) to Ayoub al-Buwati (d. 845), a student of IMAM Mohammad Idriss al-Shafi'i (767-820), founder of the Shafi'i School, the most dominant in both Zanzibar and Egypt.   Sheikh Muhsin bin Ali bin Issa Barwan taught him at the GOFU MOSQUE. He was the first ulama, who in 1944, allowed Sheikh Abdullah Saleh Farsy to teach JALALAYN at the BARZA MOSQUE during the Ramdhan. Sheikh Abdullah Saleh Farsy after studied it under Sheikh al-Amin Ali bin Abdullah bin Nafi al-Mazrui (1875-1947), who popularized the profound ideas of ISLAMIC MODERNISM as expounded by Muhammad Abduh (1845-1905), teacher of Sheikh Ahmed Muhammad Mlomry at Al-Azhar University of Egypt.   Sheikh Abdullah Saleh Farsy also received several IJAZA (Certificates) from Sheikh Umar bin Ahmed bin Abu Bakr al-Sumait (b. 1896) who taught him several books on FIQH, MANTIQ (Logic) and HADITH, among others. Unfortunately, this great ULAMA left to Yemen in 1965 due to Zanzibar dictatorship under the Christian-led government of Julius Kambarage Nyerere.
The intellectual performance of Sheikh Abdullah Saleh Farsy in secular education was equally impressive. He was so excellent in his secular education at the Central Primary School which he joined in 1924, that the English teacher did not know which specific class to enroll him. Sheikh Abdullah Saleh Farsy completed the recommended eight-year primary education for five years only.
Among his famous school teachers were Sheikh Abdullah bin Ahmed bin Seif (1900-1940) and Sheikh Abdul Bary hired by Sayyid Ali bin Humoud (1902-1911) from Al-Azhar University. For twenty years in Zanzibar, Sheikh Abdul Bary propagated Pan-Islamism and Islamic Modernism against British imperialism before the publication of QUR'AN TAKATIFU.
The QUR'AN TAKATIFU by Sheikh Abdullah Saleh Farsy was written between 1950-1967, when ideas of nationalism and secularism in Zanzibar were vague. According to Dr. Imtiyaz Yusuf, QUR'ANI TAKATIFU reflects the influences of Islamic Modernism of Sayyid Ahmed Khan (1817-1898) and Muhammad Abduh (1845-1905) as a response and component of Islamic intellectual thought in Zanzibar
But QUR'AN TAKATIFU was also a response to the Swahili translation of the Qur'an undertaken by the Rev. Godfrey Dale, a Christian Missionary in Zanzibar. His translation was meant to help the African Christian teachers employed by the University Mission to Central Africa (UMCA), founded in 1873 by the the Rev. Dr. David Livingston (1813-1873) in Zanzibar.
The translation contains 542 pages and 142 pages of comments for the (non-Arabic) text. It was published in 1923 by the London-based Society for Promoting Christian Knowledge. The translation was written according to the so called Zanzibar Swahili.
Because his translation reflected the Christian apologetics and was not acceptable to Muslims, Sheikh Mubarak bin Ahmed bin Ahmad, Head of the Ahmadiyah Muslim in East Africa started his translation in 1936 which was approved by Christian Missionaries and Orientalists in Zanzibar:  
 
    By 1942, a typescript copy was ready for submission to the Inter-Territorial (Swahili) Language for their approval. In April 1944, the Committee replied, commenting the translation as acceptable standard Swahili on the whole, with a list of proposed amendments, not all of which were adopted. The translation was then examined by a number of East African Ahamidiyas and passed by them as elegant and  tasteful Swahili. (pp. 102-103).
Sheikh Ameir bin Abeid (1924-1964), a student of Ahmadiyah in Pakistan (1954-1956) was defending the translation of the Qur'an by Ahmadiyah. But the translation of Ahmadiyah first published in 1953 aroused an uproar among the Sunni Muslims. They strongly accused Ahmadiyas of their deliberate mistranslation of certain verses to support the Ahmadiyanism. In order to challenge the Christian and Ahmadiyah translations, it was deemed essential to have an "authoritative" translation of the Qur'an. This task was shouldered by Sheikh Abdullah Saleh Farsy, who had prayed to Allah (SWT) that he should not die until he finished his Swahili Qur'anic translation.
This noble idea began when he published his first book called MAISHA YA MTUME MUHAMMAD (pbuh) which was followed by SURA ZA SALA NA TAFSIRI ZAKE (1950). Before Sheikh Abdullah Saleh expressed his criticism of the Ahmadiyah translation in booklet; UPOTOFU WA TAFSIRI YA MAKADIANI, he had already published translation and commentary of SURAH YASEEN, AL-WAQIYAH and AL-MULK with the Arabic text prior to the publication of Qadiyani in 1953. They were printed by A.A. Vasingstake in England and published in 1950 at Zanzibar.
His main translation based on the JALALAYN as his classical source, began to be published one JUZ at a time in 1956 and by 1961 twelve JUZ were published. Due to financial problem, the complete translation sponsored by the Islamic Foundation, appeared in 1969. A generous donation from the Sultan of Qatar, Sheikh Ahmed bin Ali Thani made it possible to distribute 4,000 copies free of charge and offered the remaining 3,000 copies for the reduced price of ten shillings.   Since 1950s to 1960s were the era of an intense anti-Ahmadiyah campaign by the JAMAAT EL-ISLAMI in Pakistan, the meritorious efforts of Sheikh Abdullah Saleh Farsy received a welcome support from Sheikh Abdul Maududi (1903-1979), the Chief of JAMAAT EL-ISLAMI. Despite the differences of approaches and attitudes between Islamist trends in Pakistan and in Zanzibar, Sheikh Abdullah Saleh Farsy made no distinction between Ahmadiyas and Qadiyanis as opposed in Pakistan. He simply called them MAKADIYANI (Qadianis) or MAKAFIRI (Infidels).
It was Islamic Foundation of Nairobi, an organization sympathetic to JAMAAT EL-ISLAMI, published Sheikh Abdullah Saleh Farsy's translation. Sheikh Abdullah Saleh Farsy stated that Maududi had given his personal consent for the publication of QUR'ANI TAKATIFU. Likewise, Sheikh Abdullah Saleh Farsy acknowledged the translation of Maududi's QUR'AN FAHMI KE BUNYADI USUL (Msingi wa Ufahamu Quran) and allowed his introduction of commentary TAFHIM AL-QUR'AN (1949) in QUR'ANI TAKATIFU.
After completing his Teachers Training College (TTC), Sheikh Abdullah became a primary school teacher (1932-1947) and following a series of promotions for his hard work and diligence, he was appointed the Inspector General of Primary Schools in Zanzibar and Pemba (1949-1952) by the British Colonial Administration operating from the Sultan's palaces. He was later made the Principal of the Muslim Academy Secondary School (1952-1956) before being appointed the Headmaster (1957-1960) of the Arabic Medium School. He performed HAJJ (Pilgrimage) in March 1960 and left the Ministry of Education in 1967 when he was a teacher at the Teachers' Training College.
In 1960, he was appointed as the Chief Kadhi of Zanzibar, a post he held for seven years until he migrated to Kenya. He left Zanzibar after the bloody CRUSADE in the name of the ZANZIBAR REVOLUTION on January 12, 1964 that rocked the whole African history and installed one of the most brutal dictatorships, hostile to Islamic identity in Zanzibar.
His host in Kenya was Sheikh Muhammad Kassim al-Mazrui, a lifelong friend and fellow student under Sheikh al-Amin bin Ali al-Mazrui, who taught Islam in Zanzibar. Sheikh Abdullah Saleh Farsy was no stranger in Kenya where his reputation as a leading scholar had preceded him. The retired Sheikh Muhammad Kassim al-Mazrui who recommended him to the post of Chief Kadhi of Kenya, a request that President Jomo Kenyatta (1963-1979) had no misgivings about him. For over 14 years till the time of his retirement in 1980, he was the Chief Kadhi of Kenya, a titular function he performed so remarkably.
Besides his Qur'anic translation, which is so popular that it was nearly impossible to get a copy, Sheikh Abdullah Saleh Farsy authored over 100 books and pamphlets in both Arabic and Swahili. About half of them were published but some of his published books are difficult to get them such as the IMAM SHA'FI NA WANAVYUONI WA AFRIKA MASHARIKI (Imam Mohammad Idriss al-Shafi'i (767-820), and the Great Muslim Scholars in East Africa), which qualifies to be his doctoral dissertation.  
Sheikh Abdullah Saleh Farsy passed away on November 9, 1982, barely eight months after he had left Kenya to join his family in Mascut, Oman. This death was mourned throughout East Africa. While the loss to this East African Muslim is irreparable, his legacy will remain for along time etched in memories, his accomplishments and achievements, a proud monument of his unrivalled devotion to his beloved Zanzibaris. 


(Let us pray for our Sheikh (Abdullah Saleh Farsy) with others, before and after him).
DU'A KWA SHEIKH WETU PAMOJA NA WALIOTUTANGULIA KABLA NA BAADA YAKE.

Thursday, December 12, 2013

Wahajiri wa Kiafrika wafungwa jela bila mashtaka Israel


Wahajiri wa Kiafrika wafungwa jela bila mashtaka Israel
Utawala wa Kizayuni wa Israel umewafunga jela wahajiri 480 wa Kiafrika, na idadi hiyo inaweza kuongezeka hadi kufikia 1,000 mwishoni mwa mwaka huu. Kwa mujibu wa sheria iliyopitishwa na Bunge la Israel wiki iliyopita, viongozi wa Israel wanaweza kuwaweka korokoroni wahajiri wa Kiafrika kwa muda wa mwaka mmoja bila ya kuwafungulia mashtaka. Hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel ulipitisha mpango mpya ulio dhidi ya wahajiri elfu hamsini wa Kiafrika, ambao unatoa adhabu kali dhidi ya Waafrika wanaofanya kazi huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Wakati huohuo, Taasisi ya Wahajiri ya Israel imeeleza kuwa, tokea kuanza mwaka huu wa 2013 zaidi ya wahajiri 1,600 kutoka Eritrea na Sudan wamefukuzwa huko Israel na kurejeshwa makwao. Hayo yanajiri katika hali ambayo, wahajiri wa Kiafrika wameshafanya maandamano mara kadhaa wakilalamikia vitendo hivyo vya kibaguzi na unyanyasaji, ingawa waandamanaji hao wamekuwa wakishambuliwa kwa mabomu ya machozi na risasi za plastiki na vikosi vya usalama vya Israel.

Wanamgambo wajisalimisha kwa vikosi vya UN Kongo


Wanamgambo wajisalimisha kwa vikosi vya UN Kongo
Idadi kadhaa ya wapiganaji dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wamejisalimisha kwa vikosi vya Kimataifa nchini humo. Vikosi vya Kimataifa vya kulinda amani nchini Kongo vimetangza kuwa, wapiganaji hao wamejisalimisha kufuatia operesheni kali zilizoanzishwa na majeshi hayo ya UN huko katika maeneo ya mashariki mwa Kongo na mpakani na Rwanda. Baada ya vikosi vya Kimataifa kwa kushirikiana na vikosi vya serikali ya Kongo kuwashinda wapiganaji wa Harakati ya M23 hivi karibuni, vikosi hivyo vimeazimia kuwaondoa wapiganaji wa Kihutu kutoka katika maeneo ya mashariki na katika mipaka ya pamoja na nchi ya Rwanda. Hivi karibuni Martin Kobler, Mkuu wa Operesheni ya Umoja wa Mataifa ya Kurejesha Amani nchini Kongo MONUSCO amethibitisha kuanza kwa operesheni hizo kali dhidi ya waasi wa Rwanda nchini Kongo tarehe 27 Novemba mwaka huu. Tangu mwaka 1990 mamilioni ya watu huko mashariki mwa Kongo wamekwishapoteza maisha yao kutokana na mapigano au njaa. Maeneo ya mashariki mwa Kongo yanatajwa kuwa na utajiri mwingi wa dhahabu, urani, alimasi na madini ya shaba.

Saturday, December 7, 2013

Bandar bin Sultan aendeleza njama dhidi ya Syria


Bandar bin Sultan aendeleza njama dhidi ya Syria
Bandar bin Sultan bin AbdulAziz Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Saudi Arabia ameelekea nchini Russia kwa shabaha ya kupanga mikakati mipya dhidi ya serikali ya Syria. Taarifa zinasema kuwa, safari ya Bandar bin Sultan ina lengo la kufanya njama za kukwamisha kikao cha Geneva 2 na kuimarisha nguvu za wapinzani na makundi ya kigaidi yanayopambana na serikali ya Syria. Itakumbukwa kuwa, Mwanamfalme huyo wa Saudi Arabia alionyesha radiamali kali baada ya kufikiwa makubaliano ya awali ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5 + 1 mjini Geneva hivi karibuni. Hii ni mara ya pili kwa Bandar bin Sultan kufanya safari nchini Russia katika kipindi cha miezi minne iliyopita. Katika safari iliyopita, alitoa pendekezo kwa viongozi wa Russia la kuitaka nchi hiyo iache kuiunga mkono Syria, mkabala wa Saudi Arabia kununua silaha na zana za kijeshi zenye thamani ya dola bilioni 15, pendekezo ambalo lilipingwa vikali na viongozi wa Moscow. Saudi Arabia inawapatia misaada ya kifedha na kisilaha makundi ya Geneva
Kisalafi na yale yanayowakufurisha Waislamu wengine, kwa lengo la kushadidisha machafuko nchini Syria, na hatimaye kuangushwa utawala wa Rais Bashar Assad wa nchi hiyo.

Ufaransa yaunga mkono kuundwa 'kikosi kazi' Afrika


Ufaransa yaunga mkono kuundwa 'kikosi kazi' Afrika
Serikali ya Ufaransa imeeleza azma ya kushiriki nchi hiyo kwenye uundwaji wa kikosi cha kijeshi cha Kiafrika cha kutoa radiamali haraka ifikapo mwaka 2015. Hayo yameelezwa na Laurent Fabius Waziri wa Mamb ya Nchi za Nje na Jean Yves Le Drian Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa pambizoni mwa kikao cha siku mbili cha kujadili amani na usalama barani Afrika, kinachohudhuriwa na wakuu wa nchi za Kiafrika. Wakuu wengi wa Kiafrika waliohutubia kikao hicho hapo jana  wamesema kuwa, hivi sasa Waafrika hawana uwezo wa kulinda amani na usalama wa bara hilo. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ufaransa amesema kuwa, wakuu wa nchi za Kiafrika kwa kauli moja wameafikiana  suala la kupambana na makundi ya kigaidi na maharamia katika Ghuba ya Guinea. Naye Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa amesema kuwa, kuna udharura wa kuundwa kikosi cha kutoa radiamali haraka barani Afrika kitakachokuwa chini ya usimamizi wa Umoja wa Afrika na kusisitiza kuwa, Paris inaunga mkono kikamilifu suala hilo. Jean Yves Le Drian amesema kuwa suala la maharamia katika Ghuba ya Guinea litajadiliwa kwenye Baraza la Ulaya hivi karibuni.

'Libya huenda itakabiliwa na hatima ya Somalia'


'Libya huenda itakabiliwa na hatima ya Somalia'
Rais Mahamadou Issoufou wa Niger ametahadharisha uwezekano wa Libya kutumbukia kwenye machafuko makubwa zaidi kama ilivyowahi kuikumba  Somalia. Akizungumza pambizoni mwa kikao cha usalama na amani barani Afrika huko Paris  nchini Ufaransa, Rais Issoufou ameongeza kuwa, hali ya Libya ni tete mno kwani harakati za makundi ya kigaidi na wanamgambo wa Kisalafi zinazidi kuongezeka na kuuawa makumi ya watu kila uchao katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Rais wa Niger amesisitiza udharura wa kurejeshwa amani na utulivu nchini humo. Niger ambayo inapakana na Libya upande wa kusini, imekuwa ikikabiliana na makundi yenye kuchupa mipaka ndani ya ardhi ya Niger ikisaidiana na washirika wake wa Magharibi na nchi majirani.

Wednesday, November 27, 2013

ZANZIBAR IMEZINDUA SAFARI ZA NDEGE MOJA KWA MOJA KUTOKA JOHANNESBURG AFRIKA YA KUSINI HADI ZANZIBAR.



ZANZIBAR                               
ZANZIBAR IMEZINDUA SAFARI ZA NDEGE MOJA KWA MOJA KUTOKA JOHANNESBURG AFRIKA YA KUSINI HADI ZANZIBAR.
AKIZUNGUMZA  KATIKA UZINDUZI HUO ULIOFANYIKA HOTELI YA LAGEMA NUNGWI, MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, AMELIPONGEZA SHIRIKA LA NDEGE LA MANGO KUTOKA NCHINI HUMO KWA KUAMUA KUANZISHA SAFARI HIZO.
AMESEMA SAFARI HIZO ZITASAIDIA KUONGEZA IDADI YA WATALII KUTOKA AFRIKA YA KUSINI, HASA IKIZINGATIWA KUWA WATALII WA NCHI HIYO TAYARI WAMERUHUSIWA KUINGIA NCHINI BILA YA KUWA NA VIZA.
AMEFAHAMISHA KUWA ZANZIBAR INATEGEMEA SANA SEKTA YA UTALII KATIKA KUKUZA UCHUMI WAKE, NA KWAMBA KWA SASA NDIO SEKTA KIONGOZI INAYOCHANGIA UPATIKANAJI WA FEDHA ZA KIGENI KWA ASILIMIA 72.
AMESEMA SERIKALI KWA UPANDE WAKE ITAFANYA KILA JUHUDI KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA HILO PAMOJA NA WAWEKEZAJI WENGINE, ILI KUHAKIKISHA KUWA  SEKTA YA UTALII NA UWEKEZAJI ZINAPATA MAENDELEO MAKUBWA.
AIDHA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS AMEWATAKA WATEMBEZAJI WATALII PAMOJA NA VYOMBO VYA HABARI KUWA MABALOZI WAZURI WA  KUITANGAZA ZANZIBAR KWA WAGENI, ILI KUVUTIA WATALII NA WAWEKEZAJI WENGI ZAIDI.
AMEONGEZA KUWA LENGO LA SERIKALI NI KUONA KUWA INAFANYA KAZI KWA KARIBU ZAIDI NA WENZAO WA AFRIKA YA KUSINI KATIKA SEKTA ZOTE ZA MAENDELEO, ILI KUNYANYUA HALI ZA MAISHA KWA WANANCHI WA PANDE HIZO MBILI.
KWA UPANDE WAKE BALOZI WA AFRIKA YA KUSINI NCHINI TANZANIA BW. THAMDUYCSE CHILLIZA AMESEMA WANANCHI WA AFRIKA YA KUSINI MARA ZOTE WAMEKUWA WAKIJISIFIA UKARIMU WANAOUPATA KUTOKA KWA NDUGU ZAO WA TANZANIA, NA KWAMBA HALI HIYO IMEKUWA IKIWAVUTIA WAWEKEZAJI WENGI KUTOKA NCHI HIYO.
AMESEMA UZINDUZI WA SAFARI HIZO ZA MOJA KWA MOJA UTARAHISISHA SAFARI ZA WATALII NA WAWEKEZAJI WENGINE, SAMBAMBA NA KUKUZA UHUSIANO WA MUDA MREFU ULIOPO KATI YA NCHI HIYO NA ZANZIBAR.
AMESEMA TANZANIA IMEENDELEA KUWA NCHI MUHIMU BARANI AFRIKA KUTOKANA NA UWEPO WA AMANI NA USALAMA, TOFAUTI NA ILIVYO KWA NCHI NYINGI ZA AFRIKA, HALI INAYOIPA NAFASI KUBWA ZAIDI YA KUVUTIA WAWEKEZAJI KUTOKA NCHI MBALI MBALI DUNIANI.
NAE WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, UTALII NA MICHEZO MHE. SAID ALI MBAROUK, AMEPONGEZA JUHUDI ZINAZOCHUKULIWA NA AFRIKA YA KUSINI KATIKA KUIMARISHA VITEGA UCHUMI VYAKE ZANZIBAR.
AMESEMA HATUA HIYO INADHIHIRISHA UKWELI KUWA ZANZIBAR NI MAHALI PAZURI NA SALAMA KWA UWEKEZAJI NA WAGENI, NA KULITAKIA SHIRIKA HILO LA NDEGE MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE YA KUTOA HUDUMA ZA USAFIRI WA NDEGE NCHINI.

{ZAIADA} MBAROUK SAID AMESEMA KUWA UKIMWI NI JANGA LA TAIFA HIVYO AMEWASHAURI WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA KUACHANA NA UTUMIAJI WA DAWA



WILAYA YA MJINI

AFISA UFATILIAJI WA TATHMINI YA JUMUIYA YA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA {ZAIADA} MBAROUK SAID AMESEMA KUWA UKIMWI NI JANGA LA TAIFA HIVYO AMEWASHAURI WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA KUACHANA NA UTUMIAJI WA DAWA HIZO AMBAZO KWA KIASI KIKUBWA HUSABABISHA ONGEZEKO LA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI.

AKIZUNGUMZA NA MWANDISHI WA HABARI JANA HUKO OFISINI KWAKE MWANAKWEREKWE AMESEMA KUWA NI VYEMA KWA WAZEE KUTUMIA MUDA MAALUM WA KUKAA NA WATOTO WAO KWA KUWAPA TAALUMA JUU YA ATHARI YA MARADHI HAYO AMBAYO YAMEPOTEZA MAISHA YA WATU WENGI DUNIANI HUSUSA VIJANA AMBAO NDIO TEGEMEO LA TAIFA.

AIDHA AMEFAHAMISHA KUWA JUMUIYA YAO INAENDELEA NA SHUGHULI ZA USHAURI NASAHA KWA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA NA KUWAPELEKA KATIKA VITUO VYA AFYA ILI KUWAPIMA VIRUSI VYA UKIMWI NA KUWAPELEKA KWENYE NYUMBA ZA KUREKEBISHA TABIA NA KUWEZA KUPATA UANGALIZI ZAIDI WA AFYA ZAO.

AMEFAHAMISHA KUWA JAMII SI VYEMA KUWANYANYAPAA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA NA KUWATENGA KWANI KUFANYA HIVYO KUTASABABISHA MADHARA ZAIDI KWA WATUMIAJI HAO NA BADALA YAKE KUKAA NAO PAMOJA ILI KUWAELIMISHA ATHARI ZINAZOWEZA KUWAPATA JUU YA MATUMIZI YA DAWA HIZO .

HIVYO AMEIYOMBA JAMII KUWAKUBALI NA KUWAPA MASHIRIKIANO WATU AMBAO WAMEACHA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA NA KUWASHIRIKISHA KATIKA SUGHULI ZA KIJAMII ILI KUWEZA KULETA MAENDELEO NDANI YA NCHI..