WILAYA YA MJINI
AFISA UFATILIAJI WA TATHMINI YA JUMUIYA YA KUPAMBANA NA MADAWA YA
KULEVYA {ZAIADA} MBAROUK SAID AMESEMA KUWA UKIMWI NI JANGA LA TAIFA
HIVYO AMEWASHAURI WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA KUACHANA NA UTUMIAJI WA DAWA
HIZO AMBAZO KWA KIASI KIKUBWA HUSABABISHA ONGEZEKO LA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA
UKIMWI.
AKIZUNGUMZA NA MWANDISHI WA HABARI JANA HUKO OFISINI KWAKE MWANAKWEREKWE AMESEMA KUWA NI VYEMA KWA WAZEE KUTUMIA MUDA MAALUM WA KUKAA NA WATOTO WAO KWA KUWAPA TAALUMA JUU YA ATHARI YA MARADHI HAYO AMBAYO YAMEPOTEZA MAISHA YA WATU WENGI DUNIANI HUSUSA VIJANA AMBAO NDIO TEGEMEO LA TAIFA.
AIDHA AMEFAHAMISHA KUWA JUMUIYA YAO INAENDELEA NA SHUGHULI ZA
USHAURI NASAHA KWA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA NA KUWAPELEKA KATIKA VITUO VYA
AFYA ILI KUWAPIMA VIRUSI VYA UKIMWI NA KUWAPELEKA KWENYE NYUMBA ZA KUREKEBISHA
TABIA NA KUWEZA KUPATA UANGALIZI ZAIDI WA AFYA ZAO.
AMEFAHAMISHA KUWA JAMII SI VYEMA KUWANYANYAPAA WATUMIAJI WA DAWA
ZA KULEVYA NA KUWATENGA KWANI KUFANYA HIVYO KUTASABABISHA MADHARA ZAIDI KWA
WATUMIAJI HAO NA BADALA YAKE KUKAA NAO PAMOJA ILI KUWAELIMISHA ATHARI
ZINAZOWEZA KUWAPATA JUU YA MATUMIZI YA DAWA HIZO .
HIVYO AMEIYOMBA JAMII
KUWAKUBALI NA KUWAPA MASHIRIKIANO WATU AMBAO WAMEACHA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA
NA KUWASHIRIKISHA KATIKA SUGHULI ZA KIJAMII ILI KUWEZA KULETA MAENDELEO NDANI
YA NCHI..
No comments:
Post a Comment