Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya
Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) amesema kuwa jumuia hiyo inaunga mkono
maamuzi na maazimio yaliyofikiwa katika kikao cha wakuu wa nchi za
Kiarabu na Kiafrika huko Kuwait. Samir Bakr Diab ameeleza kuwa OIC
inaunga mkono maamuzi na maazimio yaliyofikiwa katika kikao hicho cha
Kuwait khususan katika uwanja wa mapatano ya kibiashara kati ya nchi za
Kiarabu na Kiafrika na kuondolewa vizuizi vilivyopo katika uwanja huo.
Akizungumza katika kikao cha tatu cha
wakuu wa nchi za Kiarabu na Kiafrika huko Kuwait kwa niaba ya Ikmaluddin
Ehsanoghlo Katibu Mkuu wa OIC, Naibu Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Samir
Bakr Diab amesema kuwa taasisi hiyo imeanzisha mfuko wa maendeleo ya
mshikamano wa Kiislamu wenye mtaji wa dola bilioni kumi ili kuzisaidia
taasisi mbalimbali za kibiashara za nchi wanachama wa jumuiya hiyo.
No comments:
Post a Comment