Hoyce
Temu mwendeshaji wa kipindi cha Mimi na Tanzania na Juma Rashid
Mkurugenzi wa Munira Blog wakitafakari mustakbari wa mtoto Suleiman
anayesumbuliwa na ugonjwa wa ajabu.
Ndoto ya kuanza kupata matibabu na hatimaye angalau kuwa kama watoto wengine wenye kwenda watakapo inaanza kumuangazia mtoto Suleima Rajab.
Matumaini hayo yamekuja baada ya kufikishwa katika Hospitali ya CCBRT ilioyopo mikocheni Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kupata matibabu.
Munira blog ilimtembelea mtoto huyo mapema leo hii na kumkuta akiwa katika Private Ward (wodi binafsi) chumba namba tatu akiwa amekaa kitandani mwenye matumaini tele.
Bwana Rajab ambaye ni baba mzazi wa Suleiman ameiambia Munira blog kwamba wana siku ya nne tangu wafike na madaktari wamechukuwa vipimo.
"Tunasubiri matokea ya vipimo kutoka kwa wataalamu,ndipo tujuwe kinachoendelea"alisema.
Kwa upande wake Suleiman amesema anachoka kuka pamoja kwa muda mrefu na angependa aone anaanza matibabu.
Mratibu wa matibabu hayo Hoyce temu ambaye ni mwendashaji wa kipindi cha mimi na Tanzania kupitia kituo cha Channel ten amesema "tunasubiri ripoti ya madaktari ndiyo itakayotujuza mtoto Suleiman ana sumbuliwa na nini na anahitaji matibabu ya aina gani".
Naye bwana Abdul Kajumuro ambaye ni Afisa mawasiliano wa CCBRT amesema "ni vyema wananchi wakawa na subra,muda si mrefu tutapata ufumbuzi wa hili,kwani furaha yetu ni kuona mtoto huyu anakuwa kama watoto wengine".
mtoto suleiman anasumbuliwa na ugonjwa wa ajabu wa kuvimba miguu yake kadri siku zinavyokwenda.
kwa mujibu wa baba yake,mtoto huyo hajawahi kusimama dede tangu azaliwe na hajiwezi kujihudumia yeye mwenyewe hadi asasidiwe.
Mtoto Suleiman akiwa kitandani katika Hospitali ya CCBRT,nyuma yake ni baba mzazi na mbele yake ni Hoyce Temu.
Abdul Kajumuro meneja mawasiliano wa CCBRT akiwa na Mtoto Suleiman.
No comments:
Post a Comment