Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, November 1, 2013

Kiongozi wa mapinduzi Mali kupandishwa kizimbani


Kiongozi wa mapinduzi Mali kupandishwa kizimbaniKiongozi wa mapinduzi ya kijeshi yaliyoiondoa madarakani serikali ya Mali mwaka jana atapandishwa kizimbani katika mahakama moja ya nchi hiyo.
Amadou Sanogo ameitwa mahakamani kufuatia machafuko yaliyofanywa siku chache zilizopita na kundi moja na wanajeshi walioshiriki katika mapinduzi ya mwaka jana. Sanogo anahusishwa na machafuko yanayofanywa na wanajeshi waliokuwa chini ya usimamizi wake katika mapinduzi ya Machi mwaka 2012 na kwamba anapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria za kuhusika na machafuko yote yanayofanywa na kundi hilo.
Polisi ya Mali jana ilipokea kibali cha kumfikisha mahakamani Jenerali Amadou Sanogo na kibali hicho kitakabidhiwa kwa Wizara ya Ulinzi kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo. Haijajulikana bado lini Jenerali Sanogo atapandishwa kizimbani.
Machi mwaka jana Jenerali Amadou Sanogo aliongoza mapinduzi ya kijeshi yaliyoiondoa madarakani serikali ya kiongozi wa wakati huo wa Mali Amadou Toumani Toure na kukomesha kile kilichotambuliwa kuwa demokrasia iliyopiga hatua zaidi baraniA frika.

No comments:

Post a Comment