WAZIRI WA KHABARI UTAMADUNI,UTALII NA MICHEZO AL-USTADH SAID ALI MBAROUK AMEWATAKA WAZAZI NA WALEZI KUSHIRIKIANA NA WALIMU WA MADRASSA ZA QUR-AN ILI KUWAPA NGUVU KATIKA UTOAJI WA ELIMU YA QUR-AN NA SUNNA ZA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KWA VIJANA WAO.
WAZIRI MBAROUK AMETOA WITO HUO JANA KWA NIABA YA MAKAMO WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR AL-HAJJ MAALIM SEIF SHARIF HAMAD WAKATI AKIZUNGUMZA KATIKA SHEREHE ZA MADRASATUL-RAHMA YA NUNGWI WILAYA YA KASKAZINI A UNGUJA.
AMEWASISITIZA WAZAZI NA WALEZI KUWA MAKINI NA WAGENI WANAOINGIA NA MAADILI YA KIMAGHARIBI KATIKA MAENEO YAO ILI KUWAEPUSHA WATOTO WAO KUATHIRIKA NA UTAMADUNI HUO NAKUACHA MILA NA SILKA ZAKIISLAM.
AIDHA KIONGOZI HUYO AMEELEZEA HAJA KWA WAISLAM WNGINE KUFUATA MFANO WA NUNGWI KATIKA KULINDA MILA NA SILKA ZAKIISLAM KWA WATOTO WAO KWA KUANDAA SHEREHE ZA MADRASSA ZAKIISLAM ZINAZOSISITIZA MAADILI MEMA.
KATIKA SHEREHE HIZO WAZIRI MBAROUK AMEKABIDHI VIFAA NA ZAWADI MBALIMBALI IKIWEMO MIFUKO YA SARUJI KWA MADRASSA ZA NUNGWI ZILIZOTOLEWA NA MWAKILISHI WA JIMBO HILO NAKUAHIDI KUCHANGIA SHILINGI LAKI TANO KATIKA MADRASSA HIYO.
NAO WALIMU WA MADRASATUL-RAHMA YA NUNGWI WILAYA YA KASKAZINI A UNGUJA WAMEWAOMBA WAFADHILI NA WATU WENYE UWEZO KUSAIDIA HARAKATI ZA UJENZI WA MADRASSA HIYO ILI KUENDELEZA HARAKATI ZA UISLAM.
WALIMU HAO WAMETOA OMBI HILO KUPITIA RISALA YAO WALIYOISOMA MBELE YA MGENI RASMI KATIKA SHEREHE ZA MADRSSA HIYO ZINAZOFANYIKA WAKATI WANAFUNZI WANAPOINGIA KATIKA MADARASSA MENGINE.
WAMEFAFANUA KUWA MADRASSA HIYO KWA SASA INAKABILIWA NA UPUNGUFU WA VITENDEA KAZI NA UFINYU WA MADARASA YAKUFUNDSHIA.
MADRASSA HIYO ILIYOJENGWA KWA MSAADA WA SHIRIKA LA AFRIKA MUSLIM AGENCY YENYE WANAFUNZI 385 IMEANZISHWA MWAKA 1983.
No comments:
Post a Comment