Ajali iliyohusisha treni na magari mawili katika kivuko cha reli
huko Misri imeua watu 24 na kujeruhi wengine wengi. Ajali hiyo imetokea
leo asubuhi karibu na wilaya ya Giza huko Cairo mji mkuu wa Misri,
wakati treni moja ilipogongana na lori na basi dogo lililokuwa limepakia
watu wakitokea kwenye sherehe ya harusi.
Hussein Zakariya Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya Misri amesema kuwa basi dogo na lori viliparamia kwa kasi kivuko cha reli kilichokuwa kimefungwa kwa minyororo na huku kikiwa na taa za tahadhari na hivyo kusababisha ajali hiyo. Mwezi Januari mwaka huu treni moja ya mizigo iliacha njia na kusababisha vifo vya watu 17. Barabara na njia za reli nchini Misri zimekuwa na rekodi mbaya ya usalama huku wananchi wakilalamika kutokuweko na sheria msingi za usalama ili kuzuia kutokea ajali mbaya za mara kwa mara.

No comments:
Post a Comment