skip to main |
skip to sidebar
Mufti wa Libya aonya kuhusu kugawika nchi hiyo
Mufti wa Libya ametahadharisha kuhusu suala la kuifanya nchi hiyo
kuwa shirikisho katika mazingira yasiyoridhisha ya hivi sasa. Sheikh
Sadiq al Ghiryani amesema kuwa, moja ya malengo ya mapinduzi ya Februari
17 nchini humo lilikuwa ni kulinda umoja wa kitaifa wa Libya na kueleza
kuwa hali ya mambo ya hivi sasa ya Libya hairidhishi, hivyo suala la
kutaka kuifanya Libya kuwa shirikisho linalenga kuigawa vipande vipande
nchi hiyo.
Mufti huyo wa Libya amesema, kitendo cha serikali ya Tripoli cha
kutowajali wananchi, kimetoa msukumo kwa raia hao kutoa ombi hilo la
kutaka kuifanya Libya kuwa shirikisho. Ameongeza kuwa viongozi wa
serikali wanapasa kuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yao ili kuzuia
kukiukwa umoja wa mamlaka ya nchi. Wakati huohuo umoja wa maulamaa wa
Libya pia umesema kuwa, kuifanya Libya kuwa shirikisho ni kitendo
haramu na marufuku na kusisitiza kuwa mfumo wa shirikisho una madhara
makubwa kwa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment