STATE HOUSE
ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS
SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 25
Novemba, 2013
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA
LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEIPONGEZA WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI
KWA KUWEZA KUTEKELEZA KWA MAFANIKIO MAKUBWA MPANGOKAZI WA WIZARA HIYO KWA MWAKA
WA FEDHA 2012/2013.
PONGEZI HIZO AMEZITOA WAKATI AKIZUNGUMZA
KATIKA KIKAO CHA KUJADILI TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MPANGOKAZI WA WIZARA HIYO
KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013 NA TAARIFA YA ROBO YA KWANZA YA MWAKA WA FEDHA
2013/2014 KILICHOFANYIKA IKULU LEO.
DK. SHEIN ALIBAINISHA KUENDELEA KUUNGWA
MKONO NA WASHIRIKA WA MAENDELEO KWA PROGRAMU MBALIMBALI ZINAZOBUNIWA NA WIZARA
HIYO NI UTHIBITISHO WA UMAKINI WA WIZARA KATIKA KUBUNI NA KUTEKELEZA MAJUKUMU
YAKE YA KUIMARISHA KILIMO NCHINI.
HATA HIVYO MHESHIMIWA RAIS AMEITAKA WIZARA
HIYO KUONGEZA KASI YA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI JUU YA PROGRAMU ZAKE MBALIMBALI
ILI ZIWEZE KUPATA MAFANIKIO ZAIDI.
ALITOA MFANO MRADI WA UDHIBITI WA NZI WA
MATUNDA AMBAPO ALIELEZA KUWA PAMOJA NA JITIHADA ZINAZOFANYIKA ALIITAKA WIZARA
KUTOA ELIMU YA KUTOSHA ITAKAYOWAWEZESHA WANANCHI KUWATAMBUA VYEMA AINA HIYO YA
NZI NA HATUA NYINGINE ZA KUKABILIANA NAO UKIACHIA MITEGO INAYOTOLEWA SASA.
“CHAPISHENI VIJARIDA KWA LUGHA NYEPESI
KUSAIDIA WANANCHI KUWAFAHAMU NZI HAWA NA KUWAELEKEZA UMUHIMU WA KUYAFUKIA
MATUNDA YALIYOATHIRIKA BADALA YA KUYATUPA TU KITENDO AMBACHO HAKISAIDII VITA
DHIDI YA NZI HAO” DK. SHEIN ALIFAFANUA.
SAMBAMBA NA HATUA HIYO AMEITAKA WIZARA
HIYO KUIPITIA UPYA SHERIA YA UDHIBITI WA MIMEA NA MAZAO KWA KUZINGATIA
MAZINGIRA YA SASA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI.
KUHUSU SUALA LA LISHE HASA UNYONYESHAJI WA
MAZIWA YA MAMA KWA WATOTO RAIS ALIITAKA WIZARA KUELEKEZA PIA PROGRAMU ZAKE
KATIKA MAENEO YA MIJINI BADALA YA KUWEKA MKAZO ZAIDI MAENEO YA VIJIJINI KAMA
ILIVYO SASA.
“MIJINI KUNA WATU WENGI KWA MFANO MKOA WA
MJINI MAGHRIBI UNA WATU WENGI ZAIDI YA NUSU MILIONI NA WANAWAKE WENGI WA MIJINI
HAWAYONYESHI WATOTO WAO WAKATI WOTE KWA SABABU MBALIMBALI”ALIELEZA DK. SHEIN NA
KUTAKA JITIHADA ZIFANYWE KUTOA ELIMU KWA KINAMAMA HAO.
AWALI AKITOA MAELEZO KATIKA KIKAO HICHO
WAZIRI WA KILIMO NA MALIASILI SULEIMAN OTHMAN NYANGA ALIELEZA KUWA KATIKA
KIPINDI KILICHOPITA WIZARA YAKE IMEWEZA KUCHUKUA HATUA MBAMBALI ZA KUIMARISHA
KILIMO KWA KUZINGATIA MIPANGO MIKUU YA MAENDELEO NA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM.
KATIKA MWAKA WA FEDHA 2012/2013 ALISEMA
WIZARA ILICHANGIA ASIMILIA 30 YA PATO LA TAIFA AMBAPO ILIKADIRIWA KUWA ZAIDI YA
ASILIMIA 70 YA WANANCHI WALITEGEMEA SEKTA ZA KILIMO NA MALIASILI KWA AJIRA NA
MAPATO.
KWA UPANDE WA MWAKA WA FEDHA 2013/2014
WAZIRI NYANGA ALISEMA WIZARA YAKE IMEJIWEKEA MALENGO 11 ILI KUIMARISHA KILIMO
NA MALIASILI IKIWEMO KUIMARISHA MIFUMO YA KISERA NA SHERIA KWA KUZIPITIA NA
KUTAYARISHA SERA 2, SHERIA 2 NA TAFITI MBILI ZA KIUCHUMI NA KIJAMII KUKABILIANA
NA CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKTA HIYO.
MALENGO MENGINE NI KISIMAMIA UKULIMA WA
EKARI 35,000 ZA MPUNGA,KUOTESHA NA KUSAMBAZA KWA WAKULIMA MICHE MILIONI MOJA YA
MIKARAFUU, MICHE MILIONI MOJA NA NUSU YA MISITU NA MATUNDA, KUANZISHA NA
KUENDELEZA TAFITI 17 ZA MBEGU MPYA ZA UZALISHAJI WA MAZAO MAKUU YA CHAKUA NA
BIASHARA.
AKIWASILISHA RIPOTI YA UTEKELEZAJI YA
WIZARA KATIBU MKUU AFFAN OTHMAN MAALIM ALIELEZA KUWA KATIKA KIPINDI KILICHOPITA
WIZARA ILIWEZA KUKAMILISHA RASIMU YA SHERIA YA HAKIMILIKI ZA WAGUNDUZI WA AINA
ZA MBEGU ZA MIMEA PAMOJA NA RASIMU YA MPANGO WA UTEKELEZAJI SERA YA MASOKO.
KIKAKO HICHO KILIHUDHURIWA PIA NA MAKAMU
WA KWANZA WA RAIS MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD NA KATIBU MKUU KIONGOZI DK.
ABDULHAMID YAHYA MZEE.
No comments:
Post a Comment