PEMBA
MWENYEKITI WA JUMUIYA YA MAENDELEO YA ELIMU ZANZIBAR
ZEDO NDUGU USSI SAID SULEIMAN AMEWATAKA WANAFUNZI NCHINI KUSHIRIKI KATIKA
MAFUNZO YA SOCIAL MEDIA, AMEYASEMA HAYO HUKO KATIKA SKULI YA SEKONDARI UTAANI
KWENYE SHEREHE YA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA SIKU TATU YA SOCIAL MEDIA. NDUGU USSI
AMESEMA NI VYEMA KWA WANAFUNZI KUJIFUNZA UJUZI WA KOMPYUTA KWANI ITAWEZA
KUWASAIDIA IWAPO WTAITUMIA IPASAVYO. AMEWAASA WANAFUNZI KUACHA KUITUMIA
MITANDAO KATIKA MAMBO YA KIPUUZI KAMA VILE KUANGALIA PICHA ZA NGONO NA BADALA
YAKE KUITUMIA MITANDAO KWA AJILI YA KUJISOMEA. AIDHA NDUGU USSI AMESEMA ELIMU
YA KOMPYUTA IMEENEA KOTE DUNIANI. HATA HIVYO NDUGU USSI AMELIPONGEZA JESHI LA
POLISI LA MKOA WA KASKAZINI PEMBA KWA MASHIRIKIANO MAZURI WANAYOYATOA KWA
JUMUIYA YA ZEDO ILI KUONA JUMUIYA YA ZEDO INAFANIKISHA MALENGO YAKE
YALIYOJIWEKEA YA KUINUA KIWANGO CHA ELIMU KATIKA MKOA WA KASKAZINI PEMBA. NDUGU
USSI AMESEMA JESHI LA POLISI LA KUPIGWA MFANO KWA JITIHADA ZAKE KWA HALI NA
MALI ILI KUWEZA KULETA MAENDELEO MAZURI YA ELIMU KATIKA MKOA HUO. VIJANA 60 WA
MKOA HUO WAKIWEMO WANAFUNZI, WALIMU NA WAFANYA KAZI WENGINE WAMEJITOKEZA
KUSHIRIKI KATIKA MAFUNZO YA SIKU TATU YA SOCIAL MEDIA.
NAE KAMANDA WA POLISI MKOA WA KASKAZINI PEMBA RPC
BWANA MOHD SHEIKHAN MOHD, AMBAE ALIKUWA MGENI RASMI KATIKA SHEREHE HIZO ZA
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA SIKU TATU YA SOCIAL MEDIA. AMEIPONGEZA SANA JUMUIYA YA
ZEDO KWA UAMUZI WAKE WA KUANDAA MAFUNZO HAYO KATIKA MKOA HUO. AMESEMA YATAWEZA
KUWASAIDIA WANAFUNZI KATIKA MASOMO YAO. AIDHA KAMANDA MOHD AMEWATAKA WASHIRIKI
HAO KUACHA KUJIINGIZA KATIKA WIMBI LA MADAWA YA KULEVYA, WIZI NA UASHARATI NA
BADALA YAKE KUJISHUHULISHA NA MASOMO TU. AMESEMA KAMANDA MOHD NI MUHIMU SANA
KWA MAISHA YA SASA KUPATA ELIMU YA KOMPYUTA. AKIFAFANUA AMESEMA HATA MAJAMBAZI
HUTUMIA KOMPYUTA KWA MIPANGO YAO YA KUTAKA KUIBA , HIVYO ITAWEZA KUSAIDIA PIA
KUONDOSHA UHALIFU NCHINI IWAPO KUTAKUWA NA WATAALAMU WA FANI HIYO YA KOMPYUTA.
No comments:
Post a Comment