RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI
DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEIAGIZA WIZARA YA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO KUKAA PAMOJA
NA MAMLAKA YA USAFIRI WA BAHARINI KUFIKIRIA NAMNA BORA ITAKAYOWEZA KUSAIDIA
USALAMA WA WANANCHI WANAOTUMIA VYOMBO VIDOGO VIDOGO VYA USAFIRI WA BAHARINI.
DK. SHEIN AMETOA AGIZO HILO JANA WAKATI WA MKUTANO
WAKE NA UONGOZI NA WATENDAJI WA WIZARA YA MAWASILIANO NA MIUNDOMBINU KUJADILI
UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA ULIOPITA 2012/2013 NA ROBO YA KWANZA YA MWAKA WA
FEDHA 2013/2014.
AMESEMA INGAWA SHERIA ZA MAMLAKA YA USAFIRI BAHARINI
HAZIHUSISHI KAZI ZA USAFIRI WA VYOMBO VIDOGO VIDOGO, UZOEFU UMEONESHA KUWA WATU
WA MAENEO MBALI MBALI KATIKA VISIWA VYA UNGUJA NA PEMBA WANATUMIA AINA HIYO YA
USAFIRI BILA YA KUPATA USHAURI WA KITAALAMU AMBAO UTAWAHAKIKISHIA USALAMA
KATIKA SHUGHULI ZAO ZA KILA SIKU.
“PAMOJA NA KUWA SHERIA ZA MAMLAKA YA USAFIRI HAZIIPI
MAMLAKA UWEZO WA KUSHUGHULIKIA VYOMBO VIDOGO VIDOGO VYA MBAO, WANANCHI WETU
KATIKA MAENEO MBALI MBALI UNGUJA NA PEMBA WANAENDELEA KUTUMIA VYOMBO HIVYO NA
WANAHITAJI USHAURI WA KITAALAM KWA USALAMA WAO, NI VYEMA MKAKAA PAMOJA KUONA
JINSI GANI TUNAWEZA KUWASAIDIA WANANCHI WETU” ALISEMA DK. SHEIN.
ALISEMA HUU NI WAKATI MUAFAKA WA KUFIKIRIA NJIA BORA
ZITAKAZOWAHAKIKISHIA WANANCHI USALAMA IKIWA NI PAMOJA NA KUUNDA KANUNI ZA
KUSIMAMIA VYOMBO HIVYO PAMOJA NA KUWASHAURI.
VILE VILE DK. SHEIN AMEITAKA WIZARA HIYO KUCHUKUA
JUHUDI ZA MAKUSUDI KUWAELIMISHA WANANCHI JUU YA UTARATIBU UNAOTUMIKA KATIKA
KULIPA FIDIA ZA MALI ZINAZOPOTEA KUTOKANA NA UJENZI WA MIUNDO MBINU HASA
BARABARA.
AMESEMA MAENDELEO YANAKUJA NA CHANGAMOTO NYINGI AMBAZO
BAADHI YAKE ZINAKUWA VIGUMU KUKABILIANA NAZO, HIVYO BUSARA ZINAHITAJIKA ZA
KUZUNGUMZA NA WANANCHI WENYE MALI ZAO ILI WAWEZE KUKUBALI KUKABILIANA NA
CHANGAMOTO ZINAZOJITOKEZA WAKATI WA KUIMARISHA MIUNDOMBINU KWA MASLAHI YA
TAIFA.
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI
AMESEMA NI VYEMA WIZARA HIYO IKAONGEZA KASI YA KUSHUGHULIKIA MALIPO YA FIDIA
KWA WANANCHI AMBAO BAADHI YAO WAMEKUWA WAKIILALAMIKIA SERIKALI KUTOKANA NA
KUTOFAHAMU HATMA YA MALI ZAO IKIWEMO MASHAMBA NA NYUMBA.
DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEIPONGEZA WIZARA YA
MAWASILIANO NA MIUNDOMBINU KWS KUWEZA KUTEKELEZA VYEMA MALENGO YAKE
ILIYOJIPANGIA KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013
No comments:
Post a Comment