Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, November 1, 2013

Al Maliki atoa wito wa kuanzishwa vita dhidi ya ugaidi


Al Maliki atoa wito wa kuanzishwa vita dhidi ya ugaidi
Waziri Mkuu wa Iraq Nuori Al Maliki ametoa wito wa kufanyika mkutano wa kimataifa wa kupambana na ugaidi. Al Maliki ambaye alikuwa akizungumza jana katika Taasisi ya Amani ya Marekani mjini Washington amesema taifa la Iraq linalengwa na magaidi wa kundi la al Qaida ambalo linataka kufikia malengo yake kupitia njia ya umwagaji damu.
Waziri Mkuu wa Iraq amesisitiza juu ya udharura wa kuwepo ushirikiano wa kuanzisha vita vya kimataifa dhidi ya magaidi  wanaoua watu wasio na hatia.
Vilevile ametahadharisha juu ya hatari ya makundi ya kigaidi yanayoendelea kuua watu nchini Syria na kusisitiza kuwa taifa la nchi hiyo lina haki ya kuishi kwa uhuru na amani. Ametahadharisha kuwa moto na fitina za makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na nchi za Magharibi kama lile la Jabhatu Nusra huko Syria zinaweza kuyakumba maeneo na nchi nyingine dunia.

No comments:

Post a Comment