Polisi imemtia mbaroni mtuhumiwa muhimu katika tukio la mwanamke
mmoja mjini Moshi aliyetekwa nyara na watu wasiojulikana na kwenda
kutelekezwa jijini Dar es Salaam.
Mwanamke huyo alichukuliwa na watu
waliojitambulisha kuwa ni askari wa upelelezi kutoka Dar es Salaam na
kwamba, walikuwa wametumwa kumkamata kwa tuhuma za kuuza dawa za
kulevya.
Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Robert Boaz
alisema mtuhumiwa huyo muhimu (jina tunalo) alikamatwa Dar es Salaam na
kusafirishwa hadi Moshi mwishoni mwa wiki iliyopita.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 13 mwaka huu eneo la Soweto NHC, watu hao walimchukua mwanamke huyo, Asha Amini hadi Dar es Salaam na kumpora Dola 11,000 za Marekani.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 13 mwaka huu eneo la Soweto NHC, watu hao walimchukua mwanamke huyo, Asha Amini hadi Dar es Salaam na kumpora Dola 11,000 za Marekani.
Boaz alisema aliyetoa taarifa hizo polisi, ni Jerome Mushi na alijitambulisha kuwa ni mume wa mwanamke huyo.
“Aliporudi nyumbani (Mushi) hakumkuta mkewe
akaambiwa amekamatwa na polisi na amepelekwa Kituo Kikuu akaamua kwenda
hadi kituoni wakamwambia hakuna tukio kama hilo,” alisema Boaz.
Kamanda Boaz alisema jalada la uchunguzi
lilifunguliwa na siku hiyo hiyo watu walioondoka na mwanamke huyo,
walimpigia simu mumewe wakitaka walipwe Sh2 milioni.
Hata hivyo, Boaz alisema watu hao walimwachia huru
mwanamke huyo eneo la Bunju Dar es Salaam bila kumdhuru na kumpa
Sh50,000 za nauli ya kumfikisha katikati ya jiji.
Kwa upande wake, Jerome Mushi alisema waliomchukua
mkewe walikuwa na bastola moja, pingu mbili na redio moja ya upepo na
walichukua dola 11,000 za Marekani.
No comments:
Post a Comment