Mamia ya wakaazi wa mji mkuu wa
Liberia Monrovia, wamelazimika kwenda kazini kwa miguu baada ya sheria
inayoharamisha bodaboda kuingia mjini humo kuanza kutumika.
Pikipiki hizi ambazo humilikiwa na watu binafsi, hutumiwa sana na wasafiri wengi mjini Monrovia na pia katika miji mingi barani Afrika.
Baadhi ya madereva wa pikipiki hizo huwabeba hadi watu watano wakati wanaruhusiwa tu kuwabeba watu wawili.
Kwa mujibu wa taarifa ya poliisi, madereva wowote wa pikipiki hizo watakaopatikana mjini watatozwa faini ya dola miambili.
Mmoja wa madereva hao Daniel Howard alisema kuwa wameghadhabishwa mno na hatua ya serikali.
Mapema mwaka huu madereva wa Pikipiki hizo walizuiwa kuziendesha katika baadhi ya barabara za mji baada ya saa nne usiku.
Hata hivyo sheria hii ya sasa inasemekana kutatiza usafiri pakubwa mjini humo.
No comments:
Post a Comment