Ubalozi wa Iran nchini Lebanon umetangaza kwamba raia 6 wa
Kiirani ni miongoni mwa watu waliouawa katika milipuko iliyotokea nje ya
jengo la ubalozi wa Iran mjini Beirut hapo jana. Kwa mujibu wa taarifa
hiyo, Wairani hao ni Hojatulaislam Ibrahim Ansari afisa wa Kitengo cha
Utamaduni cha Iran, mke wa mwanadiplomasia wa Iran pamoja na maafisa
wanne wa usalama kwenye ubalozi huo.
Milipuko hiyo miwili iliyotokea nje ya ubalozi wa Iran mjini Beirut imepelekea watu wasiopungua 23 kuuawa na wengine 140 kujeruhiwa. Kundi la kigaidi la brigedia ya Abdullah Azzam lenye mfungamano na mtandao wa al Qaida limetangaza kuhusika na milipuko hiyo. Rais Michel Suleiman wa Lebanon amelaani milipuko hiyo na kusema kuwa serikali yake itafanya kila iwezalo kuwasaka waliohusika na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

No comments:
Post a Comment