Mamia ya wanawake wa Kenya wameandamana wakipinga adhabu ya
kufyeka majani katika ua wa kituo cha polisi waliyopatiwa wabakaji wa
mwanafunzi. Maandamano hayo yaliyofanyika katika mji mkuu wa Kenya
Nairobi yamewashirikisha mamia ya akina mama ambao wanalalamikia adhabu
ya kukata majani katika uwanja wa uwanja wa kituo cha polisi
waliyopatiwa genge lililombaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16.
Maandamano hayo yaliishia katika vituo vya polisi jijini Nairobi kwa
kukabidhi majina zaidi ya watu milioni moja yanayotoa wito wa kufanyika
uchunguzi wa kiadilifu dhidi ya kundi lililombaka msichana wa miaka 16
na kumfanyia vitendo vya kinyama. Taarifa zaidi zinasema kwamba,
msichana huyo wa miaka 16 alipigwa vibaya na kisha kubakwa na wanaume
sita wakati alipokuwa akitoka katika mazishi ya babu yake magharibi mwa
Kenya Juni mwaka huu.
Baada ya kubakwa msichana huyo alitupwa katika mtaro wa maji machafu. Kwa sasa binti huyo anatembelea baiskeli ya magurudumu kutokana na madhara ya mgongo aliyoyapa ambayo inasadikiwa yalitokana na kutupwa mtaroni au kupigwa. Polisi ya Kenya imeahidi kufanya uchunguzi kuhusiana na kesi hiyo.
…SB/habari-Ijumaa mchana

No comments:
Post a Comment