Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, November 1, 2013

Watumiaji wa Yahoo, Google waandamwa na ujasusi wa NSA


Watumiaji wa Yahoo, Google waandamwa na ujasusi wa NSA
Gazeti la Washington Post limesisitiza kuwa Wakala wa Usalama wa Taifa wa Marekani (NSA) umekuwa ukifanya ujasusi dhidi ya mamilioni ya watumiaji wa Google na Yahoo wakiwemo raia wa Marekani kwenyewe.
Hayo yanakuja katika kilele cha mgogoro mkubwa wa ujasusi wa Marekani uliofichuliwa na myaraka zilizoanikwa na mfanyakazi wa zamani wa wakala wa NSA aliyekimbilia nchini Russia, Edward Snowden.
Washington Post limeandika kuwa, wakala wa NSA unatumia programu inayoitwa MUSCULAR inayofanya kazi pamoja na programu nyingine ya Waingereza kwa ajili ya kukusanya data na ripoti za watumiaji wa Google na Yahoo.
Nyaraka za siri zinasema kuwa mwezi uliopita Wakala wa Usalama wa Taifa wa Marekani ulikusanya taarifa milioni 181 zinazojumuisha sauti, video na maandishi yanayotumwa au kupokewa na watumiaji wa intanet hususan Yahoo na Google.
Ujasusi wa Marekani katika maeneo mbalimbali dunia umezusha mvutano mkubwa kwani haukuwaonea huruma hata waitifaki wa karibu wa serikali ya Washington zikiwemo nchi za Ulaya.

No comments:

Post a Comment