Wanamgambo wa ash Shabab wamekishambulia kituo kimoja cha polisi
katika mji wa Baladweyne kaskazini mwa Mogadishu mji mkuu wa Somalia na
kuwafyatulia risasi maafisa na raia waliokuwemo ndani ya kituo hicho cha
polsi na kusababisha vifo vya watu wasiopungua kumi. Kundi la ash
Shabab lenye mfungamano na mtandao wa al Qaida limedai kuhusika na
mashambulizi hayo.
Ufyatuaji risasi uliendelea nje ya kituo cha polisi cha Baladweyne karibu na mpaka na Ethiopia kwa masaa kadhaa.
Vikosi vya Somalia vikishirikiana na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa baadaye vilikizingira kituo hicho cha polisi na kuopambana na wanamgambo hao wa ash Shabab.
Abdiasis Abu Mus’ab, msemaji wa masuala ya kijeshi wa kundi la ash Shabab amedai kuwa wanamgambo wao wameua polisi 25 wa Somalia na wanajeshi 18 wa kulinda amani wa Djibouti katika shambulio hilo la leo huko Baladweyne.

No comments:
Post a Comment