Rais Barack Obama wa Marekani na Nouri al Maliki Waziri Mkuu wa
Iraq wamekubaliana juu ya mpango wa Washington wa kuipatia serikali ya
Baghdad zana za kisasa za kijeshi kwa shabaha ya kukabiliana na makundi
ya kigaidi nchini humo. Mara baada ya kumalizika mazungumzo kati ya
viongozi hao wawili katika Ikulu ya White House, Rais Obama
alimuhakikishia al Maliki kwamba Washington itaipatia Iraq zana za
kijeshi kwa lengo la kukabiliana na makundi ya kigaidi ambayo yamekuwa
yakiendesha operesheni za kigaidi kila kona ya nchi hiyo. Kwenye
mazungumzo hayo, naye Waziri Mkuu wa Iraq amesema kuwa, demokrasia
nchini Iraq inalegalega, ingawa serikali inafanya juhudi za kuondoa
kasoro na hitilafu zilizopo. Kabla ya kuelekea Marekani, siku ya Jumanne
iliyopita Nouri al Maliki alisikika akisema kuwa, makundi ya kigaidi
kutoka nje ya nchi hiyo yameingia nchini Iraq kwa shabaha ya kufanya
ghasia na machafuko nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment