Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) amelaani
vikali vitendo vya ukatili vilivyotokea Tripoli, mji mkuu wa Libya dhidi
ya waandamanaji wasio na silaha. Mbali na Nabil al-Arab kulaani
machafuko hayo ya hivi karibuni ya mjini Tripoli ambapo makumi ya
waandamanaji waliuliwa na kujeruhiwa, amezitaka pande zote kuunga mkono
juhudi za serikali na baraza la kongresi ya kitaifa nchini humo za
kuikwamua nchi hiyo na hali mbaya iliyo nayo hivi sasa. Aidha al-Arab
ameonyesha kusikitishwa kwake na matukio hayo na akaongeza kuwa, vitendo
vya utumiaji mabavu nchini Libya vimefikia kiwango cha kutisha. Hii ni
katika hali ambayo jana baadhi ya duru za habari ziliripoti kujiri
mapigano yaliyowahusisha wakazi wa eneo la al-Shawkh huko Swalahu al-Din
katika viunga vya mji mkuu Tripoli, na wanamgambo wenye silaha. Watu 47
waliuawa na wengine 500 kujeruhiwa baada ya makundi ya watu wenye
silaha kuwamiminia risasi waandamanaji waliokuwa wakipinga vitendo vya
utumiaji mabavu nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment