Duru za habari nchini Misri zimeripoti kuwa, kwa akali wanawake
15 na wasichana 7 wenye mahusiano na kundi la Ikhwanul Muslimiin,
wanatazamiwa kupandishwa kizimbani, kwa tuhuma za kuhusika na vitendo
vya kikatili katika maandamano yaliyopita nchini humo. Habari zinasema
kuwa wanachama hao watapandishwa kizimbazi hapo kesho. Ofisi ya
mwendesha mashtaka mkuu nchini Misri imetangaza kuwa, itawafikisha
mahakamani wanawake hao ambao pia wanatajwa kuwa miongoni mwa wafuasi wa
rais aliyeuzuliwa madarakani, Muhammad Mursi, kesho Jumatano, Novemba
20, ili kujibu tuhuma dhidi yao. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, wanawake
hao walitiwa nguvuni mwishoni mwa mwezi uliopita wakituhumiwa kuhusika
na machafuko yaliyotokea katika eneo la Rushdi mkoani Alexandria.
Wasichana 7 kati ya watuhumiwa hao wanatajwa kuwa na umri kati ya miaka
18 na kuendelea na kwamba, wanaendelea kushikiliwa na vyombo vya dola
nchini Misri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment