Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, November 1, 2013

Kenya yashambulia kambi ya al Shabab Somalia


Kenya yashambulia kambi ya al Shabab Somalia
Ndege za kijeshi za Kenya zimeshambulia ngome za kundi la al Shabab ndani ya ardhi ya Somalia. Shambulizi hilo limetajwa kuwa linahusiana na hujuma ya kigaidi iliyofanywa na al Shabab mjini Nairobi zaidi ya mwezi mmoja uliopita na kuua watu karibu 70.
Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) limetangaza kuwa ndege zake za kijeshi zimeshambulia kambi ya mafunzo iliyokuwa ikitumiwa na wanachama wa al Shabab ndani ya Somalia. Shambulizi hilo linafuatia lile la Jumatatu iliyopita ambapo viongozi wawili wa kundi hilo waliuawa.
Msemaji wa jeshi la Kenya Kanali Cyrus Oguna amesema kuwa shambulizi la jana ni sehemu ya operesheni kubwa zaidi ya kikosi cha jeshi la Umoja wa Afrika AMISOM ambayo inalenga kambi za mafunzo za kundi la al Shabab. Oguna amesema watu waliofanya mashambulizi dhidi ya jumba la maduka la Westgate jijini Nairobi tarehe 21 Septemba walipata mafunzo katika kambi hiyo.
Kambi hiyo ilikuwa na wapiganaji 300 wa al Shabab na jeshi la Kenya linasema kuwa wengi wao wameuawa au kujeruhiwa.
Kanali Cyrus Oguna amesisitiza kuwa mashambulizi dhidi ya ngome za wapiganaji wa al Shabab yataendelea.
Air01/11/13 Araqchi: Urutubishaji

No comments:

Post a Comment