Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Sunday, November 3, 2013

Maharamia Somalia wamepata $ milioni 413 tokea 2005


Maharamia Somalia wamepata $ milioni 413 tokea 2005Maharamia katika Pembe ya Afrika walipata zaidi ya dola milioni 413 (Ksh Bilioni 35) kama kikomboleo kuachilia huru meli na mabaharia waliotekwa nyara tokea mwaka 2005.
Hayo ni kwa mujibu wa uchunguzi wa pamoja uliofanya na Banki ya Dunia, Umoja wa Mataifa na Interpol. Imebainika kuwa fedha za uharamia hutumika katika vitendo vya uhalifu kama vile usafirishaji haramu wa silaha na wahamiaji pamoja na kufadhili makundi ya waasi . Aidha fedha hizo pia hutumika katika biashara za kawaida kama vile  biashara ya miraa n.k. Mtaalamu wa Banki ya Dunia Stuart Yikona amepongeza juhudi za kikosi cha kimataifa cha majeshi ya wanamaji wanaokabiliana na maharamia. Ameongeza kuwa jamii ya kimataifa pia inapaswa kushirikiana ili kuzuia fedha za maharamia. Uchunguzi huo unaonyesha kuwa uharamia ni shughuli inayoratibwa kwa utaalamu mkubwa na kwamba aghalabu ya maharamia wanaendesha oparesheni zao kutoka ndani ya Somalia.
Inafaa kuashiria hapa kuwa meli za kivita za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zinalinda doria katika Ghuba ya Aden na Bahari ya Hindi kwa lengo la kukabiliana na maharamia. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya bahari IMO limepongeza mafanikio ya Jeshi la Wanamaji la Iran katika kupunguza uharamia.

No comments:

Post a Comment