Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, November 7, 2013

Mbunge Afungwa Jela


MAHAKAMA ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, imemwamuru kwenda gerezani siku 14 Mbunge wa Ukerewe, Salvatori Machemli (CHADEMA), kwa kosa la kudharau mahakama.
Machemli ambaye anakabiliwa na kesi ya uchochezi, aliamriwa kwenda gerezani jana baada ya kushindwa kuhudhuria mahakamani kusikiliza kesi yake.
Taarifa kutoka mahakamani hapo, zilisema kuwa katika kesi hiyo, Machemli anadaiwa kutumia maneno ya uchochezi katika mikutano mbalimbali ya hadhara wilayani humo mwaka jana, na kwamba amekuwa akienda nje ya wilaya hiyo na hata nje ya nchi bila idhini ya mahakama.
Inadaiwa kwamba, Machemli alipofika mahakamani hapo jana kwa lengo la kuhudhuria kesi yake hiyo, alifutiwa dhamana kisha kuamriwa kuwekwa ndani.
“Ni kweli mahakama imetoa amri ya kuwekwa ndani mheshimiwa Machemli kwa kosa la kudharau mahakama. 
Alikuwa hahudhurii tarehe za kesi yake, kutokana na hali hiyo, leo alipokuja mahakamani kuhudhuria kesi yake aliondolewa dhamana kisha akaswekwa ndani,” kilisema chanzo chetu.

No comments:

Post a Comment