Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayefuatilia masuala ya haki za
binadamu nchini Myanmar amesema kuwa fujo na ghasia dhidi ya Waislamu
zinatishia mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini humo. Tomas Ojea
Quintana amesema kuwa, kuendelea kushambuliwa na kutengwa Waislamu wa
kabila la Rohingya katika jimbo la Rakhine kunaisawiri na kutoa picha
mbaya kwa nchi hiyo na kunaitumbukiza katika hatari ya kuzuka vita
vikubwa vya kidini katika miaka ijayo. Quintana amesema inasikitisha
kuona kuwa, hata maafisa wa usalama pia wamejihusisha na vitendo vya
manyanyaso dhidi ya Waislamu na baya zaidi ni kwamba serikali imekaa
kimya bila ya kuchukua hatua zozote dhidi ya maafisa wake. Mjumbe huyo
wa UN amesema hayo mbele ya kamati ya Baraza Kuu la umoja huo
inayoendelea kupokea ripoti za hali ya haki za binadamu duniani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment