Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, November 18, 2013

Waasi wa zamani wa Seleka wamuua jaji huko CAR


Waasi wa zamani wa Seleka wamuua jaji huko CAR
Waasi wa zamani wa Muungano wa Seleka wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamewaua kwa kuwapiga risasi jaji mmoja wa nchi hiyo na mshauri wake na hivyo kuibua machafuko huko Bangui mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Mbali na kuwaua jaji huyo na mshauri wake hapo jana, raia  wengine kadhaa walijeruhiwa pia katika ufyatuaji risasi uliofanywa na waasi hao wa zamani wa Seleka  hapo jana dhidi ya wakazi wa mji mkuu Bangui waliokuwa  wakiandamana kupinga kuuliwa Jaji Modeste Martineau Bria na mshauri wake. Afisa mmoja wa polisi ya Bangui amesema kuwa Jaji Bria na mshauri wake waliuliwa kikatili na waasi wa zamani wa Muungano wa Seleka ambao waliwafyatulia risasi wahanga hao huku wakiwa wamepanda kwenye pikipiki huko katikati mwa Bangui mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Baada ya kujiri mauaji hayo, wakazi wa Bangui walimiminika mitaani na kuanza kuweka vizuizi barabarani, kuchoma moto matairi katika kupinga mauaji hayo yaliyofanywa na waasi wa zamani wa Muungano wa Seleka. Hadi sasa haijafahamika sababu halisi iliyopelekea kuuawa jaji huyo wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na mshauri wake.

No comments:

Post a Comment