Thursday, November 7, 2013
Mtoto Suleiman Hawezi Kutibiwa Nchini-Madaktari.
Hatimaye imebainika kwamba mtoto Suleiman Rajab anayesumbuliwa na ugonjwa wa ajabu,hawezi kutibiwa hapa nchini.
Kwa mujibu wa mratibu wa matibabu yake Hoyce Temu akiongea kwa njia ya simu na Munira Blog mapema leo hii amesema,madaktari bingwa wa CCBRT wamesema ni lazima mtoto huyo akatibiwe nchini India.
Amesema madaktari hao hawajawahi kufanya upasuaji wa aina hiyo kwa mtoto,kitu ambacho kimewasukuma kuchukuwa maamuzi hayo.
"Tokea jana jioni mtoto suleiman kesha toka hospitali (yupo kwao kivule) na sasa tunaanza harakati za kumpeleka india,ambapo tunaanzia kumtafutia paspoti",mwisho wa kumnukuu.
Munira blog ilimtafuta bwana Abdul Kajumuro ambaye ni meneja mawasiliano katika Hospitali ya CCBRT ili kuthibitisha hilo,ambapo alikiri kulifahamu hilo.
Aidha aliongeza kwamba "Madaktari bingwa wamekubaliana kumpeleka India kwa kuwa wenzetu wana utaalamu mkubwa na vifaa vya kutosha na tayari wameshaanza mawasiliano na madaktari wa India ili kuangalia namna ya kumsaidia mtoto huyu",alisema.
Munira blog inawaomba watu mbali mbali kumsaidia Mtoto huyu ili kufanikisha safari yake,sambamba na
kumuomba Mwenyezi Mungu ili mtoto Suleiman apate matibabu kwa wepesi na amani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment