Naibu wa Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Libya ametekwa nyara
akiwa pamoja na mmoja wa viongozi waliooongoza mapinduzi dhidi ya Kanali
Muammar Gadafi nchini humo. Televisheni ya al Jazeera ya Qatar
imeripoti kuwa, maafisa hao waandamizi wa Libya wametekwa nyara leo
mjini Tripoli. Huku hayo yakiripotiwa, habari kutoka Tripoli, mji mkuu
wa Libya zinasema kuwa, hali ya wasiwasi imerejea mjini humo baada ya
kutulia kwa muda mfupi. Kwa siku mbili mfululizo mji huo umeshuhudia
mapigano kati ya pande hasimu yaliyopelekea zaidi ya watu 40 kuuawa na
karibu laki tano wengine kujeruhiwa. Leo wananchi wa Libya wameendelea
kuwazika watu waliouawa, maziko ambayo yameambatana na maandamano ambapo
wakazi wa mji huo wameitaka serikali dhaifu ya nchi hiyo ikabiliane
vilivyo na wanamgambo wenye silaha. Wananchi hao wametishia kufanya uasi
wa nchi nzima kama serikali na makundi yenye silaha yatashindwa kufikia
makubaliano ya kurejesha amani katika nchi hiyo tajiri kwa mafuta ya
kaskazini mwa Afrika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment