
Wabunge wote wanne waliongia bungeni na vazi la Kiislamu la Hijabu ni wanachama wa chama Justice and Development Party (AKP) cha Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Hatua hiyo ambayo imepingwa na vyama vyenye mielekeo ya kisekulari, imechukuliwa mwezi mmoja baada ya serikali ya sasa ya Uturuki kufuta marufuku ya vazi la hijabu katika taasisi za serikali.
Mwaka 1999 mbunge wa kike Merve Kavakci wa chama cha Fadhila aliingia bungeni nchini Uturuki akiwa na vazi la hijabu na kuzomewa na wabunge na baadaye kuvuliwa ubunge.
Chama cha Kiislamu cha AKP kiliahidi kufuta kabisa marufuku ya vazi la hijabu nchini Uturuki wakati kiliposhika madaraka ya nchi mwaka 2002.
No comments:
Post a Comment