Maafisa wa Italia wamewatia nguvuni wahamiaji haramu 61 katika
kisiwa cha kusini mwa nchi hiyo. Kikosi cha ulinzi cha pwani ya Italia
leo Jumatatu kimewatia mbaroni wahamiaji haramu 61 waliokuwa na lengo la
kuingia katika kisiwa cha Lampedusa kusini mwa nchi hiyo. Kisiwa cha
Lampedusa kinachopatikana kati ya kisiwa cha Sicily na Tunisia hutumiwa
na makumi ya wahamiaji haramu kutoka kaskazini mwa Afrika na eneo la
Mashariki ya Kati kama njia ya kufika nchini Italia na katika nchi
nyingine za Ulaya.
Wahamiaji haramu zaidi ya elfu 36 mwaka huu wameingia Italia wakitafuta hifadhi.
Wahamiaji haramu zaidi ya elfu 36 mwaka huu wameingia Italia wakitafuta hifadhi.
No comments:
Post a Comment