Waandamanaji wanaomuunga mkono Abdulfatah al Sisi, Waziri wa
Ulinzi wa Misri wamezichoma moto picha za Waziri Mkuu wa Uturuki Recep
Tayyip Erdoğan na bendera ya nchi ya Qatar mjini Cairo, Misri.
Waandamanaji hao waliokuwa wamekusanyika mbele ya ubalozi wa Uturuki
mjini Cairo, wametaka pia kufukuzwa balozi wa Uturuki nchini kwao. Kabla
ya hapo na katika kulalamikia matamshi ya viongozi wa Ankara, Cairo
ilimuita balozi wa Uturuki nchini humo Hussein Own Butsali sambamba na
kumuondoa balozi wake mjini Ankara. Mbali na hapo serikali ya Cairo
ilitangaza kuwa, itachunguza uhusiano wake na Uturuki lakini ikatangaza
kuwa, katika hali ya sasa haitamrejesha balozi wake nchini Uturuki.
Nivyema kuashiria hapa kuwa, baada ya kuuzuliwa madarakani rais Muhammad
Mursi wa Misri, Uturuki ambayo ilikuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa
hatua hiyo, ilitangazi wazi wazi kwamba, inamtambua Mursi kuwa ndiye
rais pekee wa kisheria wa nchi hiyo. Aidha mbali na hapo Ankara
iliendelea kulaani hatua ya kuwekwa kizuizini mteja wao huyo sanjari na
kusisitiza kutaka kurejeshwa kwake madarakani nchini Misri, suala ambalo
lilizidi kupigilia msumari wa moto kwenye siasa za nchi mbili.
Inasemekana pia kwamba, Qatar ambayo ni muungaji mkubwa wa Harakati ya
Ikhwanul Muslimiin nchini Misri, ilikata misaada yake ya kifedha kwa
nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika baada ya kung’olewa madarakani rais
Muhammad Mursi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment