WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR
IMESHAURIWA KUWEKA MIONGOZO ITAKAOWAFANYA WAMILIKI WA VYUO VYA UALIMU KUSAJILI
VYUO VYAO.
MWENYEKITI WA JUMUIYA YA MAENDELEO YA ELIMU ZANZIBAR ZEDO BWANA USSI SAID SULEIMAN, AMEISHAURI SERIKALI KUPITIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR KUWEKA MIONGOZO ITAKAYOWAWEZESHA WAMILIKI WA VYUO VYA UALIMU VYA BINAFSI KUSAJILI VYUO VYAO.
USHAURI HUO AMEUTOA ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI
WA HABARI HUKO OFISINI KWAKE JADIDA WETE MKOA WA KASKAZINI PEMBA.
MWENYEKITI HUYO AMESEMA UAMUZI WA HIVI KARIBUNI WA
WIZARA YA ELIMU KUFUNGA VYUO VYOTE VYA BINAFSI VINAVYOENDESHA MAFUNZO YA UALIMU
WA MAANDALIZI HAUKUWA SAHIHI KWANI VYUO NA TAASISI ZA BINAFSI NCHINI ZINASAIDIA
SANA KUTOA FURSA MBALI MBALI ZA AJIRA KWA VIJANA.
KUFANYA HIVYO ITAPELEKEA VIJANA WENGI KUTEGEMEA AJIRA
SERIKALINI.
MWENYEKITI USSI AMBAE PIA NI MKUU WA CHUO CHA ZANZIBAR
EDUCATION COLLEGE AMESEMA NI VYEMA KWA SERIKALI KULIANGALIA KWA KINA SUALA HILO
KWANI LINAWEZA KULETA ATHARI KUBWA KWA TAIFA LETU.
TAASISI ZA BINAFSI ZIMEKUWA ZIKITOA MCHANGO MKUBWA KWA
SERIKALI HIVYO WIZARA YA ELIMU INAPASWA KUWEKA MIONGOZO MAALUM ITAKAYOWAFANYA
WAMILIKI WA VYUO VYA BINAFSI KUSAJILI VYUO VYAO.
NDUGU USSI AKIFAFANUA SABABU ZINAZOWAFANYA VIJANA
KUJIINGIZA KATIKA WIMBI LA MADAWA YA KULEVYA, WIZI NA UASHARATI NI UKOSEFU WA
AJIRA HIVYO VIJANA HUAMUA KUJIINGIZA KATIKA MATENDO MAOVU.
KUENDELEA KUWA NA CHUO KIMOJA TU AMBACHO KINATOA
MAFUNZO YA UALIMU HAPA ZANZIBAR NI KUDUMAZA MAENDELEO YA VIJANA WETU NA TAIFA
KWA UJUMLA.
KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU WAKATI UMEFIKA SASA KWA
WIZARA KUTOA VIBALI KWA TAASISI BINAFSI KUENDESHA MAFUNZO YA UALIMU HAPA
NCHINI.
AIDHA NDUGU USSI SAID SULEIMAN AMEWAPONGEZA SANA
MHESHIMIWA WAZIRI WA ELIMU NA NAIBU WAKE MHESHIMIWA ZAHRA KWA KAZI NZITO YA
KUTAKA KULETA MABADILIKO MAKUBWA YA ELIMU NCHINI INGAWA VIONGOZI HAO
WANAKABILIWA NA CHANGAMOTO NYINGI SANA.
No comments:
Post a Comment