Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, February 25, 2013

Kuna njama za kupandikiza chuki za kidini Zanzibar


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa, kuna njama za kupandikiza chuki za kidini visiwani Zanzibar huko Tanzania. Maalim Seif ametahadharisha kuwa huenda kuna watu wenye nia mbaya ambao wameamua kuyatumia matukio ya kuuawa na kujeruhiwa viongozi wa kidini, kujenga chuki baada ya kuona Wazanzibari hivi sasa ni wamoja. Maalim Seif amesema hayo alipokuwa akihutubia katika hafla ya Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), huko Wilaya ya Wete, Kaskazini Pemba. Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF amesema,

Saturday, February 23, 2013

Imamu wa Msikiti wa Mwakaje auawa

SIKU chache baada ya kutokea kifo cha Padri Evarist Gabriel Mushi na watu wasiojulikana kwa kupigwa risasi kichwani eneo la Beit el Raas, Jana Imamu wa Msikiti wa Mwakaje amefariki dunia baada ya kupigwa mapanga hadi kufa.
Kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ahmada Khamis amethibitisha kutokea kwa tukio hilo hapo jana mchana majira ya saa 8 mchana na kumtaja aliyefariki ni Sheikh Ali Khamis ambaye ameuawa na watu wasiojulikana.
Kamanda Ahmada alisema Sheikh Khamis mbali ya kuwa ni Imamu wa Msikiti lakini pia ni mkulima na ameuliwa wakati akiwa katika mazingira ya kazi zake ndani ya shamba lake huko Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Imamu wa Msikiti wa Mwakaje auawa:

 Taarifa zilizopo ni kuwa mtu mmoja anayeitwa Ali Khamis ambaye ni Imamu wa Msikiti Mkaazi wa Mwakaje amepigwa mapanga na watu wasiojulikana huko Kidoto Mkoa wa Kaskazini Unguja jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ahmada Khamis amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo anasema limetokea majira ya saa 8 mchana huko Kitope wakati Marehemu akiwa shmbani kwake, Kwa mujibu wa taarifa za polisi zinasema Imamu huyo alipigwa mapanga shingoni kwake na kupoteza damu na kusababisha kifo chake wakati akikimbizwa hospitali. Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo. Inna lillahi wainna ilayhi rajiiun.

Thursday, February 21, 2013

Jaji apinga hoja ya serikali ya kutosikilizwa kesi ya Uamsho


uamsho pix
JAJI Mkuu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Abraham Mwampashi jana anaeendesha kesi ya viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) amepinga hoja za upande wa mashataka za kutaka kutokusikilizwa ombi la upande wa watetezi wa washitakiwa kuhusu pingamizi ya dhamana.
Jaji Mwampashi alisema kuwa asingependa kupoteza muda kutokana na mambo ya kiufundi (technicality) na kama kuna pingamizi yoyote ni vizuri Serikali ipinge siku ambayo pingamizi hiyo itasikilizwa mahakamani.
Alieleza mahakamani hapo kwamba angependa kujua sababu za upande wa mashtaka kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP) kutoleta ombi lao mapema huku ikizingatiwa kuwa muda wa kesi hiyo ni mkubwa ambapo kisheria ungeanza kusikilizwa.

Sunday, February 17, 2013

DR,NCHIMBI ASEMA ”KUUWAWA KWA PADRI ZANZIBAR SI TUKIO LA KIJAMBAZI BALI NI LAKIGAIDI”



nchimbi       PADRI wa kanisa katoliki jimbo la Zanzibar,amepigwa risasi za kichwa na kifuani na kuuwawa na watu wasiojulikana.

      Padri huyo aliyetambuliwa kwa jina la Evaritus Gabriel Mushi wa kanisa katoliki parokia ya mtakatifu Joseph Shangani mjini , Zanzibar

     Watu hao ,ambao hawajafahamika wala kukamatwa ,walifanya unyama huo jana saa 12 Alfajiri asubuhi nje ya kigango cha  mtakatifu theresia kanisa la mtoni,wakati akijiandaa kushuka kwenye gari kuingia kanisani kufanya maandalizi ya ibada ya jumapili.

       Akizungumza na waandishi wa habari  kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa Alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Alisema kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maafisa wa jeshi hilo Padri Mushi ,alipigwa risasi akiwa kwenye ndani ya gari na kujeruhiwa vibaya sehemu za kichwa na kifua.
          Alisema baada ya kutokea kwa tukio hilo punde baadhi ya waumini wa kanisa hilo waliofika katika kanisa hilo  kwa ajili ya ibada walimpeleka Padri Mushi katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya matibabu baada ya muda mchache Akafariki dunia.

        “Kutokana na uzito wa tukio hili jeshi la polisi Zanzibar linaendelea na upelelezi wa kina kuhakikisha wahusika wote wanafikishwa katika vyombo vya kisheria.”Alisema kamishna Mussa

        “Natoa wito kwa wananchi washirikiane na maafisa wetu juu ya taarifa zozote zinazohusiana na tukio hili ili tuweze kutekeleza majukumu kwa wakati.” Aliendelea kusisitiza

          Kamanda wa polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ,ACP Aziz Mohamed alisema kwa sasa jeshi la polisi linaendelea na doria katika maeneo mbalimbali ya Mjini wa Zanzibar ili kuhakikisha wale wote wanaohusika katika mauaji ya padri huyo wanakamatwa.

         Wakati huo huo ,Naye Mkuu wa Mkoa Mjini Magharib Abdallah Mwinyi Amefika katika Viunga vya Hospitali ya Mnazi Mmoja Mnamo wa Saa 4 Asubuhi  kwa ajili ya kuwafariji Jamaa,ndugu na waumini wa dini hiyo waliofika katika eneo hilo kwa ajili ya kufuatilia hatima ya kiongozi wao.

           Akizungumzia tukio hilo,msemaji wa kanisa hilo ambaye pia ni katibu mkuu wa kanisa katoliki,jimbo la Zanzibar padri Cosmas Shayo aliwataka waumini wa kanisa hilo,kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki hadi suala hilo litakapotafutiwa ufumbuzi.

          Alisema Uongozi wa kanisa hilo,umepokea suala hilo kwa masikitiko makubwa pia kufariki kwa padri huyo ni miongoni mwa pigo kubwa kwa waumini na kanisa kwa ujumla.

           “Tukio hili si la kufumbia macho kwani viongozi na waumini wa kanisa katoliki Zanzibar kwasasa tunaishi kwa mashaka hali ya kuwa,mtu ukitoka asubuhi huna uhakika wa kurudi jioni ukiwa hai”Alisema padri Shayo.padri mushi
         “Kwa nini matukio haya yanaandama waumini na viongozi wa  kanisa katoliki hapa kuna agenda ya siri hadi tunafikia hatua ya kuishi kama watumwa tukiwa na hofu juu ya usalama wa maisha yetu,serikali na vyombo vya ulinzi vikiwa vinakaa kimya.”Aliendelea kusema Padri shayo.

           Alisema Kanisa linathamini mchango mkubwa uliotolewa na marehemu wakati wa uhai wake,katika kuliendeleza kanisa kwenye huduma za kiimani na kiroho kwa waumini wa kanisa.

          Baadhi ya mashuhuda ,waliozungumza kwa nyakati tofauti katika eneo la tukio ambapo walisema kwamba walifika mapema katika Kanisa hilo kwa ajili ya maandalizi ya ibada,pembeni mwa kanisa hilo kulikuwa na watu watatu ambao hawakujulikana kwa haraka ghafla baada ya kufika padri Mushi walisikia milio ya risasi wawili wakaondoka mbio na pikipiki aina ya vespa na mmoja akatokomea Vichochoroni.

          Wananchi wamesikika wakitupia lawama jeshi la polisi kwa kushindwa kudhibiti uharifu na umiliki wa silaha kinyume cha sheria,kwani matukio ya kushambuliwa kwa viongozi wa dini mbalimbali Zanzibar yameshamili.
         Wakati huo huo ,Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt, Emmanuel Nchimbi amesema serikali itahakikisha inafanya juhudi kuhakikisha inawakamata watu waliomuua Padre Evarist Mushi wa kanisa katoliki Zanzibar.

       Akizungumza na waandishi wa habari huko Makao makuu ya Polisi Zanzibar Dkt, Nchimbi amesema serikali imesikitishwa na tukio hilo alilolieleza kuwa ni la kigaidi huku akishtumu kuwa wana lengo la kuingiza nchi katika machafuko.

Amesema kuwa tukio hilo si tukio la ujambazi bali tukio la kigaidi kwani limelenga zaidi katika kuwashambulia viongozi kidini.
Amesema kuwa tukio hili limefanana na tukio lililotokea mwishoni mwa mwaka jana la kushambuliwa kwa risasi Padre Ambrose Mkenda wa Kanisa katoliki parokia ya Mpendae
Amesema kuwa katika kukabiliana na matukio ya kihalifu hapa nchini Wizara imeomba kibali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushirikia na mashirika ya kimataifa ya upelelezi ili kuwakamata wahyalifu hao.
Waumini wa Dini ya Kikiristo wakiwa katika Hospitali ya Mnazi kufuatia tukio lililotokea.
Waumini wa Dini ya Kikiristo wakiwa katika Hospitali ya Mnazi kufuatia tukio lililotokea.
Dkt, Nchimbi amewataka Watanzania kuwa wavumilivu na kujiepusha katika mtego wa kuchukia na kwa misingi ya kidini katika kipindi hichi ambacho Jeshila Polisi linaendelea na upelelezi wa tukio hilo.
Padre Evaristus Mushi ameuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana ambao walikua wamepanda pikipiki aina ya Vespa leo asubuhi wakati akielekea kuongoza misa katika kanisa la Mtakatifu Theresia la Beit el Rass.

Friday, February 15, 2013

sheikh bachu azikwa

MTAFARUKU mkubwa umezuka kati ya familia na wanafunzi wa Mwanachuoni Mkubwa wa Dini ya Kiislamu wa Afrika Mashariki, Sheikh Nassor Abdallah Bachu aliyefariki dunia jana mchana huko Chukwani Mjini Zanzibar.
Mtafaruku huo umekuja baada ya wanafamilia kuchimba kaburi mbele ya kibla cha Msikiti ambayo amesaliwa huku wanafunzi wa Sheikh huyo wakisema hawezi kuzikwa katika kibla cha Msikiti kwa kuwa ni kinyume na mafundisho ya dini ya kiislamu.
Kamati ya maandalizi ya mazishi hayo imesema kitendo kilichofanywa na wanafamilia kuchimba kaburi mbele ya msikini ni kinyume mafundisho ya dini na ni tofauti na alivyokuwa akihubiri wakati wa uhai wake ambapo mara zote alikuwa akikataza waumini wa dini ya kiislamu kuzikwa ndani ya msikiti au mbele ya msikiti.
Akiongozwa kamati hiyo, Sheikh Nurdin Kishki aliwatangazia waumini kuwa na subra wakati kamati ya maandalizi ya Sheikh huyo ikiwa ikifanya mazungumzo na wanafamilia ili kufikia mwafaka wa wapi lichimbwe kaburi lake, huku kila mmoja aliyekuwepo katika mkuanyiko huo wakisomeshana namna ya kuzikana maiti za kiislamu.
Wakati waumini hao wakitakiwa kuwa na subra baadhi ya waumini wamekwenda kulifukia kaburi la awali lililochimbwa na kusema haitowezekana kuzikwa katika eneo hilo na kutafutwa eneo jengine kwa ajili ya kuulaza mwili huo.
“Waumini tunakuombeni jamani muwe na subra lakini tunasema daima mwenyewe Marehemu Sheikh Nassor wakati wa uhai wake alikuwa akipinga suala la kuzikwa ndani ya msikiti au mbele ya msikiti lakini kaburi tunaliona limechimbwa mbele ya msikiti huku ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya kiislamu na pia ni kinyume na kile alichokuwa akikihubiri na kukisomesha, hatuwezi kuwaingilia wanafamilia kwa kuwa sisi ni wanafunzi wake tu Sheikh lakini wao ndio wenye maiti na wao ndio wenye haki lakini tunawaomba sana katika hili tusende kinyume na dini” alisema Kishki mbele ya umati mkubwa.
Baada ya vuta ni kuvute hizo wanafamilia waliingia ndani ya msikiti na kujifungia na hatimae kutoa tamko la kuuliza ni masafa gani ambayo wanataka likachimbwe kaburi na mwili wa marehemu ulazwe.
Akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari, Said Masoud Gwiji ambaye ni miongoni mwa wanafunzi wake Sheikh Nassor na pia ni mwana kamati ya maandalizi ya mazishi alisema kwamba ni vizuri wana familia wakafahamu kwamba alichokuwa akikihubiri Sheikh Nassor kiendane na kile kinachotekelzewa mwisho wa uhai wake.
Alisema sio busara kuvutana lakini kwa kuwa mafundisho ya dini ya kiislamu yanakataza kaburi kuchimbwa karibu na msikiti ni vyema likazingatiwa hilo na mazishi hayo kaburi likachimbwa kando na msikiti.
Hatimae wanafamilia na wanafunzi wa Sheikh Naassor wakakubaliana kuchimba kaburi mbali na msikiti na mazishi yakafanyika huku umati mkubwa ukiwa unashuhudia huku kila mmoja akitaka kushika maiti hiyo jambo ambalo limezusha ahama kubwa kutokana na umati mkubwa.
Naye Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad ameungana na melfu ya waumini wa dini ya Kiislamu jana katika mazishi ya Mwameanachuoni na Mhadhiri Mkubwa wa Dini ya Kiislamu Zanzibar, Sheikh Nassor Abdallah Bachu amefariki dunia juzi Chukwani Mjini Unguja.
Sheikh Nassor Bachu amefariki majira ya saa 5 mchana juzi baada ya kuugua kwa muda mrefu akisumbuliwa na kiharusi ambapo alisafirishwa kwa matibabu nchini India na katika hospitali mbali mbali za Dar es Salaam na Zanzibar kabla ya kufikwa na mauti.
Mwili wa Marehemu Sheikh Nassor ulilazimika kusaliwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja kutokana na kuwa hakuna Msikiti mkubwa ambao ungeweza kuhimili maelfu hayo ya watu waliofika kwa ajili ya kushindikiza mwili huyo.
Hii ni mara ya kwanza kwa ummati mkubwa kama huo kushiriki mazishi ya Mwanachuoni huyo ambapo awali alitakiwa kusaliwa katika Msikiti wa Kikwajuni aliokuwa akiendesha darsa wakati wa uhai wake lakini kutokana na umati mkubwa ilishindikana na kuamuliwa kusaliwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja, na baadae magari yamefuata msafara kuanzia Skuli ya Haile Sellasie na kuelekea Donge kwa kuzikwa ambapo kuanzia Mjini hadi Donge barabara imejaa wananchi wakisubiri njiani kuona msafara uliobeba maiti hiyo.
Mazishi ya Sheikh Nassor hayajawahi kutokea ambapo mbali ya ummati mkubwa kuja kushuhudia mazishi hayo wanawake na wanaume walioanzia Chukwani alipomalizikia uhai wake, na baadae kuletwa katika uwanja na Mnazi Mmoja na kupekelekwa huko Donge maelfu ya waumini wameonekana kusubiri maiti njiani na kushuhudia msafara mkubwa uliokuwa ukiongozwa na gari ya Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad.
Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Waziri wa Ofisi ya Makamo wa Pili, Mahammed Aboud Mohammed, Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi, Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Khamis Haji, Katibu Mtendaji wa Wakfu na Mali ya Amani Sheikh Abdallah Talib na Masheikh mbali mbali kutoka Nairobi, Mikoa ya Tanzania Bara, na wenyeji wao Zanzibar.
Sheikh Nassor alinza kufundisha mafunzo ya dini ya Kiislamu kwa kuendesha darsa mbali mbali katika Misikiti ya Kikwajuni na Rahaleo mnamo mwaka 1978 baada ya Mwalimu wake Sheikh Said Njugu kuanza kuumwa na kushindwa kuendesha darsa hizo ambapo majina ya wanafunzi wa Sheikh huyo yalipendekezwa matatu akiwemo Sheikh Ali Ahmad, Sheikh Othman Ali na yeye Sheikh Nassor Bachu.
Mwalimu wake Sheikh Nassor pia aliwahi kupigwa marufuku kufanya mihadhara na kuendesha darsa na Mzee Aboud Jumbe Mwinyi aliyekuwa Rais wa Zanzibar wakati huo jambo ambalo linelezwa kwamba kabla ya kifo chake Sheikh Said Njugu alikwenda kuombwa radhi na Mzee Aboud Jumbe.
Wanafunzi wa mwanzo ambayo amewasomesha Sheikh Nassor alivyoanza kuendesha darsa ambapo alianzia na wanafunzi wachache akiwemo Abdulghani Msoma ambaye ni Katibu Ofisi ya Utawala Bora, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdallah Rashid na Ali Juma Shamhuna ambaye ni waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.
Sheikh Nassor Bachu alianza kuvuma katika miaka 80 ambapo alikuwa na upinzani mkubwa kati yake na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyokuwa ikiongozwa na Rais wa wakati huo Dk Salmin Amour Juma ambapo alionekana kuhimiza wajibu na maadili ya kiislamu kufuatwa jambo ambalo lilikuwa likionekana ni geni kwa wakati huo.
Mbali kupingwa na viongozi wa serikali lakini pia Sheikh Nassor alipata upinzani mkali kutoka kwa Maulamaa na Masheikh mbali mbali wa dini ya Kiislamu kutokana na kutangaza kwake msimamo wa kufuata Sunnah -Mila za Mtume Muhammad (s.a.w) ambapo waislamu walionekana kupingana naye.
Msimamo wa Sheikh Nassor Bachu ulikuwa ni kukataza kuadhimishwa kwa kuzaliwa kwa Mtume Muhammaa (s.a.w) kwa kusomwa maulid na akitaka maadhimisho hayo yawe ni kufuata matendo yake badala ya kukusanyika, pamoja na suala la muandamo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kufuatwa popote unapoonekana jambo ambalo lilikuwa likipingwa na baadhi ya Maulamaa hapa nchini wakitaka lazima Mwezi uonekane nchini na utangazwe na serikali.
Changamoto alizokumbana nazo Sheikh Nassor katika uhai wake ni nyingi ikiwemo kutengwa na baadhi ya jamii yake, kuzuwiwa kuendesha darsa, kufungiwa misikiti asisalishe na mara kadhaa kupigwa mabomu ya machozi wakitawanywa baada ya kusali sana la Eid El Hajj ambapo hali hiyo ilianzia wakati wa utawala wa Dk Salmin na kumalizikia kwa Rais Mstaafu Amani Karume.

Tuesday, February 12, 2013

‘Sudan Kusini inapanga kuvuruga amani ya Sudan’


‘Sudan Kusini inapanga kuvuruga amani ya Sudan’Chama cha Kongress ya Taifa kinachotawala nchini Sudan, kimefichua njama iliyoratibiwa na Sudan Kusini kwa kushirikiana na Marekani na utawala haramu wa Kizayuni, kwa ajili ya kuharibu hali ya amani nchini humo. Chama hicho kimefafanua kuwa, Sudan Kusini kwa kushirikiana na Marekani na utawala haramu wa Kizayuni inafanya njama ya kuzusha machafuko katika maeneo ya Kordofan Kusini na katika jimbo la Darfur kwa kuwaunga mkono wapinzani wa serikali ya Khartoum. Aidha chama hicho kimesisitiza kuwa, njama hiyo ina lengo la kuandaa uwanja kwa Marekani na utawala ghasibu wa Israel katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuituhumu Khartoum na hivyo kupelekea kuongezwa vikwazo dhidi ya Sudan.

Tanzania yang'ara maajabu saba ya Afrika


Tanzania yang'ara maajabu saba ya Afrika
Tanzania imepata tunzo tatu za maajabu saba ya Afrika kupitia vivutio vyake bora vya utalii vya Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti ambavyo viliongoza kwa kupata kura nyingi kuliko nchi nyingine yoyote.  Akitangaza matokeo hayo mjini Arusha kaskazini mwa Tanzania mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mkuu wa taasisi iliyoandaa tunzo hiyo Dk. Phillip Imler wa Marekani, amesema, ushindi huo umetokana na kuwa Tanzania ina vivutio vya kipekee. Akielezea hifadhi ya taifa ya Serengeti, alisema kuwa ndiyo hifadhi ya kipekee iliyopata kura nyingi kutokana na tabia ya misafara ya wanyama wanaohama kwa msimu.

Kenya yapinga uingiliaji wa madola ya kigeni


Kenya yapinga uingiliaji wa madola ya kigeni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Kenya Sam Ongeri amelaani uingiliaji wa nchi za Ulaya katika masuala ya ndani ya nchi hiyo.
Ongeri amesema kuwa, wanadiplomasia wa nchi za Ulaya wanafanya njama za kuathiri matokeo ya uchaguzi ujao wa rais nchini humo. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Kenya amesisitiza kuwa, matamshi ya wanadiplomasia wa nchi hizo kuhusiana na uchaguzi ujao wa rais nchini Kenya yanachochea anga ya kisiasa nchini humo.

Sunday, February 3, 2013

NIGERIA YAKARIBISHA PENDEKEZO LA BOKO HARAM



Serikali ya Nigeria imesema kuwa ipo tayari kuangalia pendekezo lililotolewa na kundi la Boko Haram la kusitisha mapigano. Makamu wa Rais wa Nigeria Namadi Sambo amesema, Abuja inakaribisha pendekezo hilo la usitishaji mapigano la Boko Haram na kwamba serikali itajitahidi kuhakikisha kwamba amani inapatikana nchini humo. Sambo amesema hayo alipotembelea mji wa kusini mashariki mwa Nigeria wa Maiduguru ambao unahesabiwa kuwa ngome ya wapiganaji wa Boko Haram. Hii ni mara ya kwanza mji huo kutembelewa na Makamu wa Rais tangu mwaka 2009. 
Kundi lililofurutu ada la Boko Haram limehusika katika milipuko na mashambulizi tofati katika miji kadhaa ya Nigeria tangu mwaka 2009.  Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa, zaidi ya watu 1000 wameuawa kutokana na mashambulizi ya kundi hilo kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka uliopita wa 2012.

Saturday, February 2, 2013

WAZAYUNI WANADHIBITI VYOMBO VYA HABARI DUNIANI



Dakta Muhammad Sarafraz Mkuu wa Kitengo cha Matangazo ya Ng'ambo wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB amesema kuwa, mfumo wa Kizayuni unadhibiti kanali zote za habari ulimwenguni. Akizungumzia vita vipya dhidi ya vyombo vya kupasha habari vya Iran, Dakta Sarafraz amesema kuwa, iwapo itaanzishwa kanali ya habari itakayokuwa tofauti na kanali  nyinginezo, bila shaka  mfumo wa Kizayuni utaingilia kati na kuifuta kanali hiyo. Ameongeza kuwa, tarehe 28 Januari 2013 serikali ya Uhispania ilichukua maamuzi yanayokinzana wazi na uhuru wa kujieleza pale ilipotoa amri ya kukatwa matangazo ya kanali ya HispanTV ya Iran inayotangaza matangazo yake kwa lugha ya Kihispania. Dakta Sarafraz ameongeza kuwa, sehemu ya hisa ya shirika la huduma za satalaiti la Hispasat inafungamana na shirika la Eutelsat; na Mkurugenzi wa Eutelsat ni Mfaransa mweye asili ya Kizayuni ambaye hivi karibuni amekuwa akivisakama vyombo vya kupasha habari vya Iran huko Ulaya. Mkurugenzi wa Kitengo cha Matangazo ya Ng'ambo wa IRIB ameongeza kuwa, Marekani inajidai kuwa ni mtetezi mkubwa wa haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na demokrasia, amma inawaunga mkono madikteta wa Bahrain na Saudia Arabia katika kuwakandamiza wananchi wa nchi hizo.

IRAN YAONYESHA NDEGE YAKE YA KIVITA QAHER-313



Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeonyesha ndege yake ya kivita iliyotengenezwa hapa nchini ambayo uwezo wake ni sawa na ndege ya kivita ya Marekani ya F/A 18. Ndege hiyo ya kivita yenye jina la Qaher-313 yaani mshindi imeonyeshwa katika marasimu yaliyofanyika leo Jumamosi na kuhudhuriwa na Meja Jenerali Ataollah Salehi Kamanda wa Jeshi la Iran, Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi na Kamanda wa Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Brigedia Jenerali Hassan Shah Safi katika maadhimisho ya Alfajiri Kumi katika kukumbuka ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979. 

Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran amesema katika ufunguzi wa sherehe hizo kuwa ndege hiyo ya kivita ya Iran imebuniwa na kutengenezwa kikamilifu na wataalamu wa Iran.

Watu 35 wauawa katika mapigano nchini Pakistan


Watu 35 wauawa katika mapigano nchini PakistanWatu wasiopungua 35 wameuawa katika shambulio lililofanywa mapema leo na kundi la wanamgambo kwenye kituo kimoja cha upekuzi cha jeshi huko Lakki Marwat kaskazini magharibi mwa Pakistan. Kundi la Taliban ya Pakistan limetangaza kuhusika na shambulio hilo lililoandamana na ufyatulianaji risasi na uvurumishaji makombora kwenye nyumba moja. Kundi hilo limedai kuwa shambulio hilo ni jibu kwa shambulio la mwezi uliopita lililofanywa na ndege isiyo na rubani ya Marekani huko Waziristan Kaskazini na kupelekea kuuawa makamanda wawili wa kundi hilo. Msemaji wa Taliban amesema serikali ya Pakistan imekuwa ikishirikiana na Marekani katika mashambulio yake ya ndege zisizo na rubani ndani ya ardhi ya Pakistan na kwamba shambulio hilo ni la kulipiza kisasi kwa mauaji ya Faisal Khan na Toofani,

'Vikosi vya Ufaransa vitaondoka Mali kwa wakati'


'Vikosi vya Ufaransa vitaondoka Mali kwa wakati'
Rais Francois Hollande wa Ufaransa amesema vikosi vya nchi hiyo vitaendelea na operesheni zake huko kaskazini mwa Mali lakini vitakabidhi kwa wakati hatamu za uendeshaji operesheni hizo kwa vikosi vya askari wapatao 8,000 wa nchi za Afrika. Hollande ameyasema hayo leo alipokutana na vikosi vya Ufaransa huko Timbuktu wakati wa safari yake ya siku moja nchini Mali huku kukiwepo madai kwamba raia wa kawaida wameuawa kutokana na mashambulio ya anga ya Ufaransa sambamba na mauaji ya kikabila wakati wa operesheni hiyo ya kuingilia kijeshi huko kaskazini mwa Mali.

Wafungwa Waislamu UK walazimishwa kula nguruwe


Wafungwa Waislamu UK walazimishwa kula nguruwe
Haki za Waislamu nchini Uingereza zimeendelea kukiukwa huku wafungwa wa Kiislamu wanaotumikia vifungo katika magereza ya nchi hiyo wakilazimishwa kula nyama ya nguruwe. Shirika moja la kutetea haki za binadamu limetangaza kuwa, serikali ya Uingereza imekuwa ikikiuka haki za wafungwa wa Kiislamu katika magereza ya nchi hiyo. Taarifa zaidi zinasema, serikali ya Uingereza imekataa kupeleka nyama halali kwa ajili ya wafungwa wa Kiislamu katika magereza ya nchi hiyo na badala yake imekuwa ikiwalazimisha wafungwa hao wa Kiislamu kula nyama ya nguruwe ambayo kwa mujibu wa mafundisho ya dini yao ni haramu.

Friday, February 1, 2013

Jinai za kivita za Israel dhidi ya Wapalestina


Kijana Mpalestina akivunjiwa haki na wanajeshi wa IsraelWachunguzi wa haki za binaadamu katika Umoja wa Mataifa wameutaka utawala wa Israel kusitisha upanuzi wa vitongoji vya waloezi wa Kizayuni na kuwaondoa walowezi nusu milioni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Katika taarifa iliyotolewa Alkhamisi jopo la Umoja wa Mataifa limesema hatua ya kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina ni jambo ambalo linaweza kuhesabiwa kuwa jinai za kivita. Ripoti hiyo imeongeza kuwa ulowezi wa Wazayuni umechangia ukiukaji wa haki za Wapalestina kwa njia nyingi.

Vita vya Ufaransa Mali: Haki za binaadmau zakiukwa



Wanajeshi wa Ufaransa nchini Mali 
Shirika la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch limetaka uchunguzi ufanyike kuhusu vitendo vya ukiukwaji wa haki za binaadamu vinavyotendwa na vikosi vya kijeshi vinavyoongozwa na Ufaransa nchini Mali.
Mkurugenzi wa Human Rights Watch barani Afrika Tiseke Kasambala ametoa taarifa na kuvitaka vikosi vya Ufaransa kupunguza ukatili na mauaji ya raia Mali.
Ufaransa ilianzisha vita dhidi ya Mali karibu mwezi mmoja uliopita kwa kisingizio cha kupambana na magaidi kaskazini mwa nchi hiyo. Tayari wanajeshi kutoka Niger na Togo wameshajiunga na vikosi vya Ufaransa katika vita nchini Mali. Imearifiwa kuwa mji wa Gao sasa unadhibitiwa na vikosi vya Ufaransa baada ya kushikiliwa na waasi kwa muda wa miezi 10. Nchi zinazounga mkono vita vya Ufaransa nchini Mali ni pamoja na Marekani, Canada, Uingereza, Ubelgiji, Ujerumani na Denmark. Weledi wa mambo wanasema lengo la vita vya Mali ni kupora utajiri mkubwa wa mali asili nchini humo kama vile mafuta, dhahabu na madini ya urani.

Wasiwasi wa UN kuhusu harakati za al Shabab Somalia

    Waasi wa al Shabab, Somalia
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa wapiganaji wa kundi la al Shabab wanagali wanaendeleza harakati zao Somalia jambo ambalo linaweza kuwa kizingiti katika marekebisho ya kisiasa na kiusalama nchini humo.
Katika taarifa Umoja wa Mataifa umesema baada ya kumalizika malumbano ya kisiasa Somalia mwaka 2012 tishio kubwa zaidi sasa ni kundi la kigaidi la al Shabab.
Wakati huo huo Mkuu wa Masuala ya Kisiasa katika Umoja wa Mataifa Jeffery Feltman amesema umoja huo umejizatiti kusaidia Somalia kujenga amani ya kudumu. Ameyasema hayo Alkhamisi mjini Mogadishu baada ya mazungumzo yake na vinogozi wa Somalia.

Waislamu Tanzania kujadili kadhia ya Sheikh Ponda



Sheikh Ponda akifungwa pingu mahakamaniViongozi wa taasisi kadhaa za Kiislamu Tanzania wameitisha mkutano wa hadhara kwa lengo la kujadili kadhia ya Sheikh Ponda Isa Ponda anayeshikiliwa korokoroni.
Taarifa zinasema kuwa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu pamoja na Shura ya Maimamu Tanzania imeitisha mkutano Jumapili Februari 3 saa nne mchana. Mkutano huo umepangwa kufanyika katika Kiwanja cha Nuurul Yaqiin karibu na Uwanja wa Mwembe Yanga mjini Dar-es-Salaam
Imearifiwa kuwa mkutano huo unatazamiwa kuonyesha mshikamano wa Waislamu na Katibu wa Jumuia na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa ambaye anakabiliwa na kesi ya uchochezi. Walioandaa mkutano huo wanalalamika kuwa Sheikh Ponda na wenzake wamenyimwa haki ya dhamana na wanateseka jela. Kesi ya Sheikh Ponda ilisikilizwa jana Alkhamisi na inatazamiwa kuendelea Februari 18 mwezi huu.

Shahidi adai kina Ponda walivamia eneo




(TANGAZO LA KONGOMANO La Waislamu Jumapili ya Februari 3.)

MLINZI wa Kampuni ya Agritanza Ltd, Julius Mlanzi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jinsi kundi la Waislamu lilivyofika na kutaka warejeshewe eneo La Makazi lililopo Chang’ombe, mali ya waislamu.

Mlinzi huyu Alidai mahakamani kuwa Waislamu hao Wamemtaka mmiliki wa eneo hilo kuwasiliana na aliyemuuzia ili arejeshewe fedha alizotoa kwa madai wao wamefika kuchukua mali yao.

Katika kesi hiyo, Sheikh Ponda issa Ponda, na, Shekhe Mukadam Abdallah Swalehe na waislamu wengine 48 wanakabiliwa na mashtaka manne, likiwamo la uchochezi na wizi wa mali yenye thamani ya Sh59.6 milioni.