skip to main |
skip to sidebar
MUUNGANO HARAMU
Kuna adhimu ujumbe, mwapaswa kuufahamu
Ni wajibu niulumbe, mpate kuufahamu
Chanzoche Aboud Jumbe, ' PARTNERSHIP ' fahamu,
... ' Kitaka kuufahamu, msome Aboud Jumbe.
Kimechambua kimbembe, Cha muungano haramu,
Ulosheni upambe, wa kambi mbili hasim
Zote za nyundo na jembe, japo moja madhulumu, ' Kitaka kuufahamu, msome Aboud Jumbe.
Yatakwa funikwa kombe, apite mwanaharamu
Au ridhaa iombe, kwa mshirika adhimu
Nyayoze 'kibidi' rambe, kwa khushui na nidhamu,
' Kitaka kuufahamu, msome Aboud Jumbe.
La sivyo wake viumbe, washikezao hatamu,
Vinginevyo chembechembe, huingizwa zenye sumu,
' Kitaka kuufahamu, msome Aboud Jumbe.
Uhai sasa wa tembe, muungano haramu,
Kisa wa watu upambe, waso na yake elimu,
Mithili ya wanywa pombe, waso vichwani fahamu, ' Kitaka kuufahamu, msome Aboud Jumbe.
Umriwe si ukembe, mkongwe ni wa kadimu
Nilolenga si upembe, nikuzindua kaumu,
ILi watu wasiyumbe, kwa muungno haramu,
' Kitaka kuufahamu, msome Aboud Jumbe.
Kitabu kina ujumbe, maridhia kwa kaumu
Kutoka kwa ' Bwana ' Jumbe, Kiongozi muadhamu,
Kimelifunua kombe, asipite mwanaharamu
' Kitaka kuufahamu, msome Aboud Jumbe.
Kaditamati ujumbe, sina zima kwa kaumu
Kadhalika mze Jumbe ashatimiza jukumu
Mwisho nyote niwaombe, someni zake salamu,
"""""KITAKA KUFAHAMU, MSOME ABOUD JUMBE"""""
No comments:
Post a Comment