Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya
zanzibar (SMZ), Ali Juma Shamuhuna, amesema kuwa na mawazo ya kuvunja
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar sawa na kujichimbia kaburi.
Shamuhuna alitoa tamko hilo katika kikao cha pamoja cha ushirikiano kati ya Wizara yake na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya Serikali ya Muungano, mjini hapa juzi.
Alisema kwamba kama Muungano wa Tanganyika na Zanzibar una kasoro dawa yake ni kuzitatua kwa maslahi ya pande mbili za Muungano na sio kuwa na fikra za kuuvunja kwani umeleta amani na umoja wa kitaifa kwa Watanzania.
“Kuwa na mawazo ya kuvunja muungano sawa na kujichimbia kaburi,…Sisi tuliouganishwa katika muungano tunapaswa kulinda na kuuendeleza muungano wetu,” alisema Waziri Shamuhuna.
“Mawaziri tuna jukumu kubwa sana mie sikubaliani na wale wanaosema muungano hauna faida yoyote,” alisema Waziri Shamuhuna ambaye pia mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa.
Aidha, alisema kwamba Wizara yake itafanyakazi kwa karibu na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya Muungano ili kuharakisha kiwango cha ubora wa elimu kinaendelea kuimarika Tanzania Zanzibar.
Tangu kuanza mijadala ya katiba mpya kumeibuka kikundi cha wanaharakati Zanzibar ambao wanashawishi wananchi kuvunja Muungano na kutoa lugha chafu dhidi ya waasisi wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar na viongozi wa kitaifa Zanzibar.
Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Serikali ya Muungano, Dk Shukuru Kawambwa, alisema wanafunzi 12,269 wameshindwa kupata mikopo ya elimu ya juu kutokana na Serikali ya Muungano kukosa fedha za kugharamia elimu katika mwaka wa fedha 2011/12.
Dk Kawambwa alisema jumla ya wanafunzi 38,541 walifanyiwa udahili na kuonekana wanazo sifa na vigezo lakini wanafunzi 26,272 tu ndio walionufaika na mikopo ya elimu ya juu. Aidha alisema kwamba serikali imeshindwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wenye sifa kutokana na ufinyu wa bajeti yake

No comments:
Post a Comment