Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, May 7, 2012

RISALA KWA ZINJIBARI




1. Risala wa Zinjibari milele utumikao
Ngiya kachika bahari umtumai Molio
Nusura ndako Ghafari waja utunusuruo
Kwa qadha ipisiyeo hayasii mayutoye!

 

6. Yatakapo kuwaswibu tuli hai duniyani
Mutakutwa ni aibu ya dhila na nukhusani
Mutoleweo naswibu watoovu wa imani
Ole wenu fahamuni hayasii mayutoye!

 

7. Ole wenu fahamuni watumbuizi wa ole
Mumengiya ghafulani musaliyeo wavule
Ghamidha yenu na k’ani hizayae nda milele
Vuwani mato muole hayasii mayutoye!

 

12. Nanyi mufurahiyeo ni watovu wa fikira
Nyungu muwandishiyeo haikupuwa tijara
Muruwa wenu na cheo mumeuza kwa khasara
Wala hapana nusura hayasii mayutoye!

 

13. Wala hapana nusura wapungufu wa aqili
Muivutiye izara na kukosa t’ajamali
Khila zenu na busara ndiwo msinji wa dhuli
Kumbukani ya aswili hayasii mayutoye!

 

15. Nanyi musiyo laiti haya muyachendeeo
Sitiraji na waqati umeondoka si yeo
Yadhihiripo mauti furahaze ni kilio
Munao ole munao hayasii mayutoye!

 

16. Munao ole munao mungatimba lenu shimo
Hawangii pweke yao nanyi mutangiya momo
Mangi muyachendeeo yasokuwa na ukomo
Mfupi na mwenye kimo hayasii mayutoye!

 

19. Zizi mutiziye tuwi khasara hiyo nda ng’ombe
Hono ni mwiso mwiwi fahamiyani dhiumbe
Mvunda kwao hakuwi huwa kama seserumbe
Kisima cha t’imbet’imbe hayasii mayutoye!

 

21. Kwa nyoyo dhenu dhaifu mutakiona kichendo
Deuli kwa masanafu zisiwatie mishindo
Mungawa hai muwafu simba kuvundakwe ondo
K’aa akosapo gendo hayasii mayutoye!

No comments:

Post a Comment