Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi
na Vyombo vyote
vya Dola
wafanye kazi zao kama wanavyotakiwa kwa mujibu
wa muongozo
wa haki za binadamu kwa Polisi na vikosi vingine
unaosema kwamba
polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu
la kutunza amani
na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu.
Kila mtu anayo
haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya kitaifa na
kimataifa yatakayomuwezesha
kupata haki zake za binadamu.
vya Dola
wafanye kazi zao kama wanavyotakiwa kwa mujibu
wa muongozo
wa haki za binadamu kwa Polisi na vikosi vingine
unaosema kwamba
polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu
la kutunza amani
na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu.
Kila mtu anayo
haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya kitaifa na
kimataifa yatakayomuwezesha
kupata haki zake za binadamu.
JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA
YA KIISLAMU
(JUMIKI)
للجنة الدعوة
الإسلامية
THE ASSOCIATION FOR
ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266
-Tel: +255-777-419473 / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail:
jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI ZANZIBAR
Tarehe 27MAY2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Kila sifa njema anastahiki ALLAH
(S.W) na Rehma na Amani zimuendee Mtume Muhammad (S.A.W), ahli zake, Maswahaba
zake na walio wema katika Uislamu.
Jumuia ya UAMSHO inatoa taarifa
rasmi kwa umma wa Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kwamba haihusiki na
vitendo vyote vya uvunjaji wa amani vilivyotokea usiku wa tarehe 26 Mei 2012.
Kama alivyosema Mtume (S.A.W) katika Hijatul Wadaa, kwamba ni haramu kumwaga
damu zenu, kuharibiana mali zenu, kuvunjiana heshma zenu ila kwa haki ya Uislamu
(maana yake pale mtu anapofanya kosa na likathibitika atahukumiwa kwa hukmu ya
Kiislamu). Vile vile Uislamu unaheshimu nyumba za ibada (Makanisa, Mahekalu na
n.k) zisivunjwe wala zisiharibiwe.
Jumuia inatoa wito kwa Waislamu
na Wazanzibari wote kuendelea kudumisha amani na utulivu wa nchi na kutoharibu
mali za serikali, mali za wananchi, mali za taasisi za dini zenye imani tofauti,
kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya Kiislamu. Jumuiya
inayachukulia matukio yaliyotokea usiku wa jana, na yanayoendelea tangu alfajiri
leo, kama ni njama za makusudi za wale wasioipendelea amani nchi hii, pamoja na
kutaka kuipaka matope jumuiya na kutaka kuzuia lengo la Wazanzibari kudai nchi
yao.
Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi
na Vyombo vyote vya Dola wafanye kazi zao kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa
muongozo wa haki za binadamu kwa Polisi na vikosi vingine unaosema kwamba polisi
na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la
kutoingilia haki za watu. Kila mtu anayo haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya
kitaifa na kimataifa yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu.
Polisi na vyombo vingine vya
dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za
watu isipokuwa tu kwa minajil ya kulinda haki za wengine.
Polisi na vyombo vingine vya
dola wana jukumu la kuheshimu, kulinda na kutetea haki za binadamu kwa watu
wote.
WABILLLAH
TAWFIQ
No comments:
Post a Comment