KUNA WANAODHANI WANAWEZA TENA KUTUGAWA WAZANZIBAR KWA KUTUMIA MBINU ZILIZOPITWA NA WAKATI ZA ETI KUSEMA KIZAZI CHA SULTANI KINAJIPENYEZA KUTAKA KURUDI KUITAWALA ZANZIBAR HUU NI UJINGA NA KUTOKIKUJUWA WANACHOKISEMA NA ZAIDI HAWAIJUI HII ZANZIBAR WAPI IPO NA ILIPITA WAPI WAPI!
Walitakiwa wajuwe kwanza ni sababu gani iliyomfanya mfalme wa Oman kuja Afrika Mashariki na kamuondoa Mreno.
Wareno walipoizuru pwani ya Afrika Mashariki mwaka wa 1498 wakiongozwa na Vasco da Gama katika juhudi yao ya kutafuta njia ya Bahari ya kufika Bara Hindi, walistaajabu sana kuona kuwa takriban watu wote wa Afrika Mashariki walikuwa ni Waislamu.
Baada ya miaka michache walipofaulu kuiweka Afrika Mashariki chini ya himaya yao, walianza harakati za kuuondoa Uislamu kwa njia yoyote waliyoweza kutumia. Waislamu wa Afrika Mashariki, kuona wanaendelea kunyanyaswa, walikata shauri ya kutafuta msaada wa kijeshi kutoka nchi yoyote ya Kiislamu ili wamwondoe Mreno. Mikutano ya siri baina ya Waislamu na makabila mengine ya Afrika Mashariki ikawa ikifanyika kutoka Lamu Kaskazini mpaka Kilwa Kusini ya upwa wote. Mwisho wakakata shauri kupeleka ujumbe wa siri kwa mfalme wa Oman kutaka msaada wake. Ujumbe wenyewe ulikuwa ni wa watu wanane, ukiongozwa na Mwinyi Nguti wa Mwinyi Mwinzagu, Mzee wa Waswahili wa Mombasa. We n g i n e w a l i k u w a n i Mwishahali bin Ndari, Maalim Ndao bin Haji, Mwinyi Mole bin Haji, Sheikh Ahmed AllMalindi na Mtomato wa Mtorogo wote wa Mombasa, Kubo wa Mwamzungu ambaye alikuwa mzee wa Kidigo miongoni mwa makabila ya Mijikenda ya pwani ya Kenya na Shahame bin Shoka aliyewawakilisha watu wa kisiwa cha Pemba.
Ujumbe uliondoka Mombasa mwaka wa 1660 na ukapokewa kwa taadhima na Mfalme wa Oman aliyekuwa akiitwa Imam Sultan bin Seif Al-Yaarubi. Mwaka wa 1661 Jeshi la mabaharia na askari wa KiOman lilihujumu na kuteka mji wa Mombasa lakini hawakuweza kuwafukuza Wareno, Imam Sultan alifariki.
O m a n i l i k a b i l i w a n a mapigano ya wao wenyewe kwa wenyewe. Baada ya miaka kumi hivi mtawala mpya akawa mwanawe Imam Sultan aliyeitwa Seif bin Sultan AlYaarubi, “Qaid-ul-Ardh” Qaid ul Ardh akadhamiria kumaliza kazi ilioanzishwa na marehemu baba yake ya kuwaondoa Wareno. Akabuni jeshi kubwa la majahazi 18 yaliyobeba askari 3,000 kutoka makabila mbali mbali ya Mashariki ya kati, Makabila ya Ki-Oman kama vile Mazrui, Mundhry, Jeneby, Shikely, Bassamy na Maamry, askari wa kiajemi na askari wa kibulushi. Amir Jeshi aliyechaguliwa na Qaid-ul-Ardh alikuwa ni jemedari maarufu wa Ki-Baluchi kutoka pwani ya Makaran katika jimbo la Baluchistan la Uajemi.
Jemedari huyo alikuwa akiitwa Jemedar Amir Shahdad Chotah. Chotah akauteka mji wa Mombasa lakini kwa vile Wareno wote wa Mombasa wapatao 2,500 walijifungia ndani ya Ngome ya Mombasa, hakuweza kuiteka ile ngome. Chotah aliizunguka Ngome hiyo kwa muda mrefu, Jeshi la Jemedari Chotah lilifanikiwa kuiteka Ngome hiyo baada ya miezi 33. Jemedari Chotah akawapata Wareno wanane tu na Waswahili wachache. Wengi wa Wareno waliuwawa na kukimbia kuelekea Msumbiji, hawakuweza kurudi tena. Wengi wa makabila ya watu wa Oman waliuwawa katika mapigano ya kuwakomboa ndugu zao wa Kiislamu chini ya utawala wa Wareno. Kuanzia hapo ndio watu wanyewe kwa ridhaa zao wakataka ulinzi wa watu wa Oman na hapo ndipo palipozidi kuoana baina ya Waswahili na watu wa Oman. Sio rahisi hivi sasa kuweza kuwatenganisha Wazanzibari na wa Oman kwa vile ni watu wamoja ki-damu na ki-dini.
No comments:
Post a Comment