JUMUIYA ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) Zanzibar imesiistiza kuendelea na harakati zao za kutoa elimu ya uraia licha ya serikali kupiga marufuku mihadhara hiyo. Kwa mujibu wa barua yenye kumbukumbu namba JMK/OUT/VOL-12/2012 ya Mei 09 mwaka huu imesema huu sio wakati wa kulazimishana na kuwataka viongozi wa nchi kuheshimu mawazo ya wananchi wanaopinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
“Huu sio wakati wa kulazimisha watu Muungano kuukubali au kuukataa watu wapewe uhuru wa kura ya maoni kila mtu aamue kwa uhuru wake” imesema barua hiyo ambayo mwananchi imepata nakala yake.
Tamko ya Jumuiya hiyo limekuja siku moja baada ya kauli ya Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein kutoa kauli ya kuwataka watu ambao wamechoshwa na amani iliyopo kuhama nchi.
“Jumuiya inachukua fursa hii kuwanasihi viongozi kuacha kutumia madaraka vibaya na kuwakumbusha ibara ya 12 ya katiba ya Zanzibar “watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote” hivyo watawajibika kwa utumiaji wowote mbaya wa madaraka yao pia tunawakumbuka maneno ya Mheshimiwa Shein aliyoyasema katika jimbo la Koani ….”endeleeni kuitunza amani ya Zanzibar aliyechoka na amani aondoke ahame kabisa atuachie….” ilisema barua hiyo ya Uamsho.
Hata hivyo katika kusisitiza na harakati zao jumuiya hiyo imewataka waislamu nchini kuungana na wenzao waliopo kisiwani Pemba kujumuika katika sala maalumu itakayosaliwa leo katika viwanja vya Tibirinzi Chake Chake Pemba.
“Jumuiya kwa mnasaba huu inachukua fursa hii kuwatangazia waislamu na wazanzibari kuwa itafanya dua kisiwani Pemba pamoja na sala ya Ijumaa tarehe 11 mwezi huu hapo Chake Chake ikifuatiwa na mihadhara wilaya zote za Pemba inshallah” imesema taarifa hiyo iliyotolewa kwa waandishi wa habari.
Barua hiyo ambayo nakala zake imepelekwa kwa Rais wa Zanzibar, makamo wa kwanza na makamo wa pili wa rais wa Zanzibar, mwanasheria mkuu waziri wa sheria na katiba wakuu wa mikoa jeshi la polisi na idara ya Mufti imesema kila mzanzibari afahamu kuwa aha haki kamili ya kuabudu, kueneza dini, uhuru wa maoni, uhuru wa kujumuika, kupata habari na taarifa kuzipokea na kuzitoa.
Huku wakinukuu vifungu vya sheria viongozi wa jumuiya hiyo ambao wamesema wataendelea na harakati zao kama kawaida licha ya kutoka agizo la serikali linalowataka kuacha kufanya mihadhara na mikusanyiko ya katiba wakati huu ambao watanzania wanaelekea kwenye mchakato wa ukusanyaji wa maoni ya katiba mpya ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa, na Mkuu wa Kaskazini Pemba wamepiga marufuku mihadhara ya aina yoyote ya inayozungumzia masuala ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amri hiyo imetolewa mbele ya kamati ya ulinzi na usalama iliyohudhuriwa na Masheha na viongozi wengine wa serikali ambapo wamesema ni marufuku kwa mihadhara inayozungumzia masuala ya muungano kufanyika katika mikoa yote ya Pemba.
Wakuu wa mikoa hao kwa pamoja wamesema Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar, ndiyo iliyopiga mafuruku mihadhara hiyo, kwani suala la mchakato wa katiba halina ruhusa ya kuzungumzwa hadi kupatikane kwa kibali kutoka tume inayoratibu masuala hayo.
Katika kukazia suala hilo wakuu wa mikoa hao amewataka masheha na wakuu wa wilaya zote, kutokuruhusu kufanyika kwa mihadhara inayozungumzia masuala ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika shehia zao.
Sambamba na hilo sasa ni marufuku kuangalia DVD za jumuiya hizo ambazo hufunguliwa na kutazamwa katika maeneo mbali mbali kwenye vibanda vya video na amri hiyo imewaagiza jeshi la polisi kuzikusanya DVD hizo na kuzidhibiti zisisambazwe.
Wakitoa angalizo kwa watendaji wao wakuu wa mikoa hao wamesema iwapo kutafanyika mkusanyiko au mhadhara wowote bila ya sheha kuripoti taasisi zinazohusika au polisi basi sheha huyo atawajibika kisheria.
Wakijibu amri hyo ya kudhibitiwa kwa DVD Jumuiya hiyo wamesema wamefuata taratibi zote za kisheria na kufuata katiba ya Zanzibar bila ya kukiuka katika kusimamisha mihadhara.
Walisema jumuiya inasikitishwa sana na jeshi la polisi kuburuzwa na wakuu wa mikoa na kukubali kushiriki katika uvunjifu wa amani na ukiukwaji wa katiba ambapo walisema wanashangazwa wakati katiba inaweka wazi na kubainisha haki na uhuru wa kuabudu na kueneza dini kama ibara ya 19 inavyoeleza.
“Tunapenda ifahamike kwamba jumuiya ilifuata taratibu zote za kisheia na kufuata katiba ya Zanzibar bila ya kukiuka katiba kusimamia mihadhara hiyo” ilisema tarifa hiyo.
“Tunashangaa sana wakati katiba ya Zanzibar imeweka wazi na kubainisha haki na uhuru wa kuabudu nakueneza dini kama ibara ya 19 inavyooleza ,kila mtu anastahiki kuwa na uhuru wa mawazo ,wa imani, kazi ya kutangaza dini kufanya ibada na kueneza dini itakuwa huru ,shughui na uwendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi”.
Katika hatua nyengine Jumuiya hiyo inakusudia kumfikisha mahakamani Mwanasheria mkuu wa serikali kwa tuhuma za uvunjifu wa amani na ukikwaji wa katiba ya Zanzibar.
Taarifa ya jumuiya hiyo imesema itamfikisha mahakamani baada ya kupata ushauri kutoka kwa wanasheria mbali mbali kutokana na ukiukwaji wa katiba ya Zanzibar unaofanywa na kikundi cha watu wachache wasioitakia mema Zanzibar na wanaotumia madaaka yao vibayan kwa maslahi yao binafsi.
Hayo yamebainishwa katika tarifa yake iliyotolewa na kusambazwa katika vyombo vya habari kutokana na kauli ya mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba Dadi Faki Dadi kupia marufuku mihadhara inayosimamiwa na jumuiya ya Uamsho na mihadhara ya kislamu Zanzibar .
Taifa hiyo ilisema “Inaonyesha kuna ajenda ya siri iliyokabidhiwa kikundi cha watu wachache akiwemo Makamo wa pili wa rais Balozi Seif Ali Iddi,akifuatiwa na wazirri katika Ofisi yake Mohammed Aboud pamoja na kumuamuru Mhe Soraga katibu wa Mufti na kumburuza katika uvunjifu wa amani
No comments:
Post a Comment