Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Saturday, May 12, 2012

MISUKO SUKO ILIO IKUMBA SEAGULL



Seagull yazimika Nungwi yapotelea Tanga
Ilikuwa na abiria 300 ikitokea Pemba

Tokea maafa ya MV SPICES zaidi ya mara tatu kumetokea matokeo mbali mbali kuhusu meli na boti za abiria,na hakuna juhudi za aina yoyote zilizochukuliwa kuimarisha usafiri wa baharini,ndugu wananchi Mwenyezi Mungu atunusuru lakini Mwenyezi Mungu anasema jisaidie nikusaidie na mpaka sasa inavyoonekana sisi wenyewe hatujisaidii haya yote ni maonyo kubwa linakuja Allah atuepushie hili na lile.



ABIRIA... 300 waliokuwemo katika meli ya MV Seagull wakitokea kisiwani Pemba kuelekea Unguja jana, walipatwa na hofu kubwa baada ya meli hiyo kuzimika katika mkondo wa Nungwi na kubururwa na maji hadi Tanga.

Baada ya taarifa hizo Kampuni inayomiliki MV Seagull ilitoa meli yake nyengine SKAGIT ili kwenda kuisaidia meli hiyo katika namna itayoona inafaa.

Lengo la meli hiyo lilikuwa ni kufika na kuifunga meli hiyo ili kuiburura, kwani ingekuwa vigumu kuruhusu abiria kuingia katika meli hiyo kwa vile hali hiyo ingesababisha hatari zaidi kutokana na watu wengi wangetaka kuingia kwa hofu waliyokuwanayo.


Kabla ya meli hiyo kurudi kulipatikana taarifa kwamba mashine ya MV Seagull imewaka huko Tanga, baada ya kufanyiwa matengenezo hivyo kuweza kurudi Unguja yenyewe na abiria iliyokuwanayo wakiwa salama.

Tukio hilo liliripotiwa mapema jana mchana baada ya abiria waliokuwemo ndani ya meli hiyo kuwapigia simu jamaa zao kuwapa taarifa hiyo, hali ambayo ilizua hofu kwa ndugu na jamaa zao hao.

Kutokana na taarifa hizo wananchi kadhaa walijazana katika bandarini kusubiri jamaa zao baada ya kupata taarifa ya kuzimika meli hiyo.

Wakizungumzia kuharibika huko, wananchi wamesema kuzimika kwa meli hiyo mara kwa mara ikiwemo safarini na abiria, pamoja na nyengine zenye kufanya safari za Unguja na Pemba ni hatari ambayo inaonekana kueleweka lakini hakuna njia zinazoonekana kuchukuliwa kuondosha tatizo hilo.

Baadhi ya wananchi waliokuwa wakisubiri jamaa zao wamesema kwamba kuna haja ya Serikali kununua meli kubwa ya abiria na mizigo kwa ajili ya kusafirisha wananchi Unguja na Pemba, ambapo usafiri wa baharini ni wa lazima.

Aidha walieleza kushangazwa kwao kuruhusiwa meli hiyo kupakia abiria wakati ni hivi karibuni ilizuiliwa kwa kutokamilisha taratibu za kusafirisha abiria ikiwemo ubovu.

Tokea kuzama kwa MV Spice Islanders Septemba mwaka jana, wananchi wa Zanzibar wamekuwa wakisafiri kwa hofu katika meli zinazotoa huduma hivi sasa ambapo mara kwa mara zimekuwa zikiharibika.

Katika nyakati tafauti na viongozi tafauti wa kitaifa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imekuwa ikieleza kwamba inaendelea na mpango wa kutafuta meli mpya ya kupakia abiria na mizigo ili kuwaondoshea wananchi usumbufu wa usafiri

No comments:

Post a Comment