Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, August 6, 2012

WAZANZIBAR WAMEOMBA DUWA

Duwa imefana

Mamia kwa maelfu ya Wazanzibar wamejitokeza kwenye Duwa ya pamoja ya kuliombea Taifa ikifuwatiwa na vijinjo kwa ajili ya Kafara kwa kila aliekalia vibaya Taifa la Zanzibar.

  watu ni wengi na bado waliendelea kufuri kakatika Msikiti huu wa Afrah Bint Issa Kidongo Chekundu Mjini Zanzibar.

Msikiti ulijaa na watu wengi wameonekana nje ya eneo la Msikiti

Kiongozi wa Duwa hii ni Sheikh Mussa Juma, muhadhiri wa Jumuiya ya Muamsho na Imam wa Msikiti wa Biziredi.


Wanyama hawatochinywa hapa na badala yake watachinywa Kisakasaka machinjio ya Serikali.


Waislaam karibia ya wote  machozi yaliwatoka kwa duwa zilizoombwa hapa. Jamhuri ya Watu wa Zanzibar,,,,,
 
 
 Duwa iliendelea

  mpaka kfika zamu ya Amir Farid na hapo na akaatowa waadhi,  anasema "nawashukuru sana wale wote waliotowa sadaka zao, kwa upande wa ng'ombe walikuwa ni ng'ombe wa nane na mbuzi 35; pia jana katika kusadifia tarehe zote mbili jana tulifanya duwa msikiti wa Mbuyuni na jana Sheikh Habib Ali kombo aliongoza duwa msikiti Gofu.

Pia tulipokea kuku 21, bata 1 na njiwa 1.

Moja katika vita vinavyopigwa ni vita vya propaganda, kwa hiyo sisi tukishatowa taarifa tujuwe kuwa sisi viongozi tumeshaamuwa na wala msitupigie simu kutuuliza kuwa duwa ipo, pia mkitumiwa mesji msizisambaze, na hapa tushasema sensa hatushiriki kwa hiyo msitupigie simu kutuuliza sensa ipo.

Pia Waziri wa Katiba alipotwambia kuwa sensa itakuwa siku moja sisi tulimwambia kuwa sisi hatutaki sensa tunataka nchi yetu kwa hiyo siku tutayoipata nchi yetu tutaeka siku moja ya hiyo sensa.

Hakuna serikali hata moja duniani iliyowahi kuwa juu ya wananchi na siku zote serikali hushindwa na wananchi. Moja kati ya serikali iliyokuwa na nguvu ilikuwa ni serikali ya Iran wakati wa Shaa alipeleaka vifaru kuwapiga wananchi lakini walivyokuta kuwa umma ni mkubwa walitupa silaha zao chini.

Tunawaomba wale wote waliohudhuria hapa wakiondoka waondoke kwa amani, pia tunalitaka jeshi la polisi lichunge amani, wananchi waliokuwepo hapa walikuja kwa jili ya duwa

Kuna propaganda zinatolewa huko nje wanasema wale wanachinja na kuchinya ni haram nawaomba muachane na maneno hayo, Allah anasema na ,mkichinya mchinje kwa ajili ya Allah, na tumekatwawa kuchinja kwa asiekuwa Allah.

Tunawaomba waumini warejee kwa amani na salama na tukipita mabarabarani tupite kwa salama na tuzitumie kwa uzuri na tunajuwa kuwa waislaam ni watu wa amani.

Viongozi wameshauri jambo moja na wametaka ridhaa yenu, kuwa nyama hii wagaiwe watoto mayatima, kisha wagaiwa watu wazima, kisha wangaiwe na wanawake."
Watu wote wameridhika.

Sheikh Farid alimaliza kwa duwa 

1 comment:

  1. ﻋﻨﺪ ﻣﻮﺗﻚ ﻻ ﺗﻘﻠﻖ
    ﻻ ﺗﻘﻠﻖ ﻭﻻ ﺗﻬﺘﻢ ﺑﺠﺴﺪﻙ ﻓﺎﻟﻤﺴﻠﻤﻮﻥ ﺳﻴﻘﻮﻣﻮﻥ ﺑﺎﻟﻼﺯﻡ:
    ☇ ﻳﺠﺮﺩﻭﻧﻚ ﻣﻦ ﻣﻼﺑﺴﻚ
    ☇ ﻳﻐﺴﻠﻮﻧﻚ
    ☇ ﻳﻜﻔﻨﻮﻧﻚ
    ☇ ﻭﻳﺨﺮﺟﻮﻧﻚ ﻣﻦ ﺑﻴﺘﻚ ﺇﻟﻰ ﺣﻔﺮﺗﻚ ) ﻗﺒﺮﻙ (
    ﻭﺳﻴﺄﺗﻲ ﺍﻟﻜﺜﻴﺮﻭﻥ ﻟﺘﺸﻴﻴﻊ ﺟﻨﺎﺯﺗﻚ ﺑﻞ ﺳﻴﻠﻐﻲ ﺍﻟﻜﺜﻴﺮ
    ﻣﻨﻬﻢ ﺃﻋﻤﺎﻟﻪ ﻷﺟﻞ ﺩﻓﻨﻚ ﻭﻗﺪ ﻳﻜﻮﻥ ﺍﻟﻜﺜﻴﺮ ﻣﻨﻬﻢ ﻟﻢ ﻳﻔﻜﺮ
    ﻓﻲ ﻧﺼﻴﺤﺘﻚ ﻳﻮﻣﺎ ..
    ﺍﻏﺮﺍﺿﻚ ﺳﻴﺘﻢ ﺍﻟﺘﺨﻠﺺ ﻣﻨﻬﺎ
    ☇ ﻣﻔﺎﺗﻴﺤﻚ
    ☇ ﻛﺘﺒﻚ ﺷﻨﻄﻚ
    ☇ ﺍﺣﺬﻳﺘﻚ ﻣﻼﺑﺴﻚ
    ☇ ﻭﺍﻥ ﻛﺎﻥ ﺍﻫﻠﻚ ﻣﻮﻓﻘﻴﻦ ﻓﺴﻮﻑ ﻳﺘﺼﺪﻗﻮﻥ ﺑﻬﺎ ﻟﺘﻨﻔﻌﻚ
    ﻭﺗﺄﻛﺪ ﺑﺄﻥ:
    ☇ ﺍﻟﺪﻧﻴﺎ ﻟﻦ ﺗﺤﺰﻥ ﻋﻠﻴﻚ!
    ☇ ﻭﺍﻟﻌﺎﻟﻢ ﻭﺍﻹﻗﺘﺼﺎﺩ ﺳﻴﺴﺘﻤﺮ!
    ☇ ﻋﻤﻠﻚ ﺳﻴﺄﺗﻲ ﻏﻴﺮﻙ ﻟﻴﻘﻮﻡ ﺑﻪ!
    ☇ ﺃﻣﻮﺍﻟﻚ ﺳﺘﺬﻫﺐ ﺣﻼﻻ ﻟﻠﻮﺭﺛﺔ
    ☇ ﻭﺃﻧﺖ ﺳﺘﺤﺎﺳﺐ ﻋﻦ ﺍﻟﻨﻘﻴﺮ ﻭﺍﻟﻘﻄﻤﻴﺮ!
    ﺍﻟﺤﺰﻥ ﺃﻧﻮﺍﻉ:
    ☇ ﺍﻟﻨﺎﺱ ﺍﻟﺬﻳﻦ ﻳﻌﺮﻓﻮﻧﻚ ﺳﻄﺤﻴﺎ ﺳﻴﻘﻮﻟﻮﻥ ﻣﺴﻜﻴﻦ!
    ﺃﺻﺪﻗﺎﺅﻙ ﺳﻴﺤﺰﻧﻮﻥ ﺳﺎﻋﺎﺕ ﺛﻢ ﻳﻌﻮﺩﻭﻥﺇﻟﻰ ﺳﻮﺍﻟﻔﻬﻢ
    ﻭﺿﺤﻜﻬﻢ!
    ﺍﻟﺤﺰﻥ ﺍﻟﻌﻤﻴﻖ ﻓﻲ ﺍﻟﺒﻴﺖ!
    ☇ ﺃﻫﻠﻚ ﺇﺳﺒﻮﻉ ﺇﺳﺒﻮﻋﻴﻦ ﺷﻬﺮ ﻭﻣﻦ ﺛﻢ ﺳﻴﻀﻌﻮﻧﻚ ﻓﻲ
    ﺍﻷﺭﺷﻴﻒ
    " ﺇﻧﺘﻬﺖ ﻗﺼﺘﻚ ﺑﻴﻦ ﺍﻟﻨﺎﺱ "
    ☇ ﻟﻦ ﻳﻨﻔﻌﻚ ﻣﺪﺡ ﺍﻟﻨﺎﺱ ﻳﻮﻣﺌﺬ
    ☇ ﻭﻟﻦ ﻳﻀﺮﻙ ﺫﻡ ﺍﻟﻨﺎﺱ ﻳﻮﻣﺌﺬ
    ﻭﺑﺪﺃﺕ ﻗﺼﺘﻚ ﻣﻊ ﺍﻵﺧﺮﺓ
    ☇ ﻭﺍﻟﺴﺆﺍﻝ ﺍﻟﻤﻄﺮﻭﺡ :
    ☇ ﻣﺎﺫﺍ ﺃﻋﺪﺩﺕ ﻟﻘﺒﺮﻙ ﻭﺁﺧﺮﺗﻚ ̣'
    ﻳﺎﺭﺏ ﺍﺣﺴﻦ ﺧــﺘـﺎﻣـﻨـﺎ ﻳــﺎﺭﺏ
    ﻭﻛﻞ ﻣﻦ ﻗﺎﻝ ﺍﻣﻴﻦ

    ReplyDelete