Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, August 16, 2012

Zanzibar itakuwa kijiji cha wavuvi

Haljazaul ihsan il-lal ihsan,Mheshimiwa Mzee Wetu Hassan Nassor Moyo kwa dhati ya moyo wetu tunasema jazaka llahu -kheir,Tunauthamini sana mchango wako nasi tuko pamoja nawe kwa hali na mali.
Mwenye macho haambiwi tizama huona kwa macho yake hali kadhalika mwenye masikio husikia kwa masikioye.
Wengi wamejitokeza kama Ali Mohamed Ameir
Mohamed Seif Khatib na wenginewe watajitokeza lakini wote hawawi mfano wako ,kwa ukweli na ushujaa Mola akuhifadhi kwani yeye Mola ndie kinga yetu sote.
Viongozi wote wa zanzibar waliojitokeza kuungana na wananchi wa visiwa hivi ikiwa kutoka CCM au CUF
wameonyesha ujasiri ,ukakamavu ,ushujaa na ukweli katika kulitetea Taifa la Zanzibar tunawaunga mkono na tunaahidi tutakuwa nao bega kwa bega katika kufanikisha uhuru kamili wa kujiamulia mambo yake wenyewe ya kitaifa na kimataifa.
Wale wabunge walioongozwa na Mohamed Seif Khatib huko dodoma hawako kwa ajili ya wazanzibari wako kwa ajili ya dodoma na ikiwa wapo kwa ajili ya zanzibar na waje zanzibar na watoe tamko hilo wakati wakiwa hapa zanzibar vyenginevyo tunajua wako kwa ajili ya dodoma na wazanzibari hawatasikiliza dodoma kwa sasa masikio ya wazanzibar yapo chukwani na sio dodoma
Ikiwa wabunge wote 30 walifatana na Mohammed Khatib wamechaguliwa zanzibar na wanazungumzia matakwa ya wazanzibari ,hao wabunge hawakutimia idadi ya wabunge wa zanzibar ,wabunge wa zanzibar zaidi ya 50 hivyo hao wachache hawataweza kutoa kauli kwa zanzibar ,
Wazanzibari tunataka kura ya maoni kuhusu mustakbali wa nchi yetu na tumetuma mapendekezo mara kadhaa katika baraza la wawakilishi sasa ikiwa Mohamed seif Khatibu ni msema kweli na yupo katika bunge kama ni muwakilishi wa zanzibar na apeleke utetezi wetu wa wazanzibar kwanza wanataka kura ya maoni.la ikiwa ni kwa manufaa yao binafsi na utashi wa kisiasa na hawataweza kutusemea wazanzibari itakuwa hawana maana ya kuwepo katika bunge ikiwa kuwepo kwao ni kwa kuwakemea wanaotaka serikali ya mkataba na kweli zanzibar inatakikana serikali ya mkataba na wao sio watetezi wa hiyo serikali ya mkataba nawajisarambatishe mapema kabla hawajasarambatishwa na jamii ya wazanzibari.
Wazanzibari wa leo sio wa jana na wa kesho sio wa leo kila siku vijana wanakuwa ngangari kila viongozi wakichelewa katika maamuzi ya kuipatia zanzibar mamlaka yake kamili mambo yanakuwa mengine mfano wake kama mwizi kila akiwa anakimbia na mbio nyingi ndio anazidi kuwakusanya watu wa kumkamata na kumpa kipigo takatifu.
Maoni yanatolewa na wazanzibari na kila kukicha maoni yanazidi kupamba moto ,maoni tunayoyataka kuyasikia ni ya serikali ya mkataba na alhamdulillah wazanzibar wameyafahamu na hawatochangia lengine lolote lile kwani ni kupanda katika tume ya kukusanya maoni na kusema nataka serikali ya mkataba (full stop)
Hapo tena ikishapatikana serikali ya mkataba ndipo tutasema raisi awe na vichwa kumi au kimoja ,raisi asiwe na mke kwani anaweza kushauriwa vibaya na mkewe,tena hapo tutasema tutakavyo,la umuhimu ni kupita katika serikali ya mkataba na ndio msimamo kamili.
Asilimia 75 kusini pemba imetupa moyo kuwa mambo kweli yamefahamika kwani itakapokuja mjini magharibi (aso mwana aeleke jiwe)asilimia 99.99 hiyo moja itakayokosekana itakuwa ya Mohamed Abuod na akiwa amefahamu maana ya mamlaka kamili basi itakuwa asilimia 100-Inshaalla atafahamu.
Wazanzibari lazima tuwe kitu kimoja na wale ambao hawakufahamu waelimishwe ili wafahamu kama sheha wa donge anao muelekeo wa kufahamu karibuni hivi.
Nia yetu ni kuwa na serikali yetu jamhuri ya zanzibar tena hapo kila ambacho tunahitaji tutakipendekeza katika serikali yetu ili kuinua maisha ya wazanzibari.
Bila ya kuwa na jamhuri ya zanzibar kwa muungano huu feki hatufiki pahali,kero zitazidi umasikini utatumaliza tahamaki zanzibar itakuwa kijiji cha wavuvi.

No comments:

Post a Comment