Waaislamu nchini Zanzibar wametakiwa wasishiriki sensa kwani ndani ya sensa kuna mtego ambao utasababisha madhara makunwa dhidi ya waislamu.
Hayo yameelezwa na amiri wa jumuiya hiyo Sh Mselem bin Ally katika mkutano ambao uliwashirikisha waandishi wa habar ambao ulifanyika katika viunga vya msikiti wa mbuyun zanzibar kwa lengo la kutoa tamko la waislamu kwa nini wanakataa sensa.
Akibainisha miongoni mwa sababu ambazo zinawafanya wasikubali sensa ni pamoja na kuondoshwa kipengele cha dini licha ya kwamba Serikali imejitetea kwa kudai ya kwamba wao hawapangi mambo ya maendeleo kwa kuzingatia dini, jambo ambalo si kweli bali ni kuendeleza ile desturi ya serikali ya muungano katika kutii matakwa ya maelekezo ya ya mfumo Kristo ambao umekua ukiendesha Serikali hiyo kwa maslahi ya makanisa na wakiristo kwa muda mrefu.
akiongezea amesema wazanzibar na waislamu hawashiriki sensa mpaka yafanyike mambo yafuatayo;
1-Wazanzibar wote wenye haki ya kisheria wapatiwe vitambulisho vya Uzanzibari na wale wote wasiostahiki wakapewa kwa utashi wa kisiasa virejeshwe.
2-Wazanzibar wana vitambulisho vyao kwa hiyo vitambulisho vinavyotoka Tanganyika kwa jina la Tanzania visitishwe mara moja kuletwa Zanzibar.
3-Ili wazanzibar washiriki sensa kwanza wapatiwe nchi yao ya Zanzibar yenye mamlaka kamili iksha watajihesabu.
4-kipengele cha dini kiingizwe katika dodoso la sensa kwani hili si geni katika sheria za kimataifa za sensa ili kujua nchi inaendeshwa vipi ili kuchunga maslahi ya wenye dini zao.
5-Serikali zote mbili zitoe tamko la kulaani vitendo vya jeshi la polisi vya kinyama vya kunajisi miskiti na kuharibu nyumba za ibada kama walivyolaani wakati yalipoharibiwa makanisa na hatimae kuzawadiwa nafasi ya uwakilishi katika baraza la uwakilishi.
6-vyombo vya habari (ikiwemo ZBC) vilivoripoti taarifa zisizo sahihi na kuwachafua JUMIKI ndani na nje ya nchi iwaombe radhi waislamu kwa kupotosha habari kitu ambacho kimewasababishia wapate maafa makubwa.
Kutokana na mikakati hiyo wazanzibar wametakiwa wasusie zoezi la sensa hadi pale madai yao yatakaposikilizwa na kufanyiwa kazi kwa uakmilifu wake. kwa hiyo kila mwenye uchungu wa Zanzibar na chembe ya imani ya Uislamu haimfalii kushiriki zoezi la sensa kwani kufanya hivo ni kuusaliti Uislamu na kuisaliti Zanzibar.
No comments:
Post a Comment