Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, August 30, 2012

Malawi yajiondoa kwenye Paralympics

Malawi imejiondoa kutoka mashindano ya Olimpiki ya walemavu yaliyoanza rasmi mjini London.
Hii ingekuwa mara ya kwanza kwa taifa hilo kushiriki katika michezo hiyo lakini inadaiwa kuwa ukosefu wa fedha umeilazimisha kujiondoa.
Wanariadha vipofu Chisomo Jeremani na Janet Shedani pamoja na wasaidizi wao wawili na maafisa wanne wa michezo ndio waliotarajiwa kusafiri London kwa ajili ya michezo hiyo.
Kamati ya michezo ya olimipiki ya walemavu nchini humo, imelaumu serikali pamoja na makampuni ya kibinafsi kwa kukosa kuwafadhili.
Kamati ya kimataifa ya Paralimpics huenda ikapendekeza hatua kuchukuliwa dhidi ya Malawi.
Waandalizi wa michezo hiyo nchini Uingereza, Locog tayari walikuwa wametoa ufadhili kusaidia katika safari ya wachezaji hao kuelekea London,lakini kulingana na maafisa nchini Malawi, pesa hizo hazikutosha kutuma kikosi chote hicho ikiwemo wanariadha na wasaidizi wao.
Mwandishi wa BBC nchini Malawi, Frank Kandu amesema kuwa changamoto zinazokabili kamati ya michezo ya paralympics ya Malawi, zilisababishwa na matatizo ya kiuchumi yanayoikabili nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.
Mnamo mwezi Mei, rais mpya wa nchi hiyo Joyce Banda, alishusha thamani ya sarafu ya nchi hiyo kwa asilimia 33 kama sehemu ya mpango wa serikali kutaka jamii ya kimataifa kuanza tena kuipatia msaada.

No comments:

Post a Comment