WARIDI LA: 1
Omba Tawbah sana kwa Allaah سبحانه وتعالى Na jiweke katika Twaharah daima
}}...إِنَّ اللّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ{{
{{…… Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha}}
Al-Baqarah:222
WARIDI LA: 2
Mfuate Mtume صلى الله عليهو آله وسلم kwa kutimiza Sunnah zake na fuata tabia na mwendo wake ili uthibitishe mapenzi yako kwa Allaah سبحانه وتعالى .
}}قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَاللّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ {{
{{Sema:
Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi
Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni
Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu}}
Al-Imraan:31
Vile vile fuata Sunnah za Makhalifa Wanne waliongoka, Abubakar, 'Umar, 'Uthmaan na 'Aliy
عنهما رضي الله
.
WARIDI LA : 3
Timiza
Fardhi yako kwanza vizuri, kisha ongeza na Sunnah zaidi za Swalah,
kutoa sadaqa, kwenda Umra, kufanya kila aina ya wema kwa wazazi na
Waislamu wenzako.
((عن أبي هريرة رضي الله عنه قال
قال رسول الله صلى الله عليه وآله وسلم إن الله قال من عادى لي وليا فقد آذنته بالحرب وما تقرب إلي عبدي بشيء أحب إلي مما افترضت عليه وما يزال عبدي يتقرب إلي بالنوافل حتى أحبه فإذا أحببته كنت سمعه الذي يسمع به وبصره الذي يبصر به ويده التي يبطش بها ورجله التي يمشي بها وإن سألني لأعطينه ولئن استعاذني لأعيذنه وما ترددت عن شيء أنا فاعله ترددي عن نفس المؤمن يكره الموت وأنا أكره مساءته))
قال رسول الله صلى الله عليه وآله وسلم إن الله قال من عادى لي وليا فقد آذنته بالحرب وما تقرب إلي عبدي بشيء أحب إلي مما افترضت عليه وما يزال عبدي يتقرب إلي بالنوافل حتى أحبه فإذا أحببته كنت سمعه الذي يسمع به وبصره الذي يبصر به ويده التي يبطش بها ورجله التي يمشي بها وإن سألني لأعطينه ولئن استعاذني لأعيذنه وما ترددت عن شيء أنا فاعله ترددي عن نفس المؤمن يكره الموت وأنا أكره مساءته))
((Inatoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه ambaye alisema: Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema: Yeyote yule afanyae uadui kwa walii (rafiki) wangu nitatangaza
vita dhidi yake. Mja wangu hanikaribii na kitu chochote ninachokipenda
kama amali nilizomuwajibisha, na mja wangu huzidi kunikaribia kwa amali
njema za Sunnah ili nimpende. Ninapompenda huwa (Mimi ni) masikio yake
anayosikilizia, macho yake anayoonea, mikono yake anayopigania, miguu
yake anayokwendea, lau angeniomba kitu bila shaka ningempa, lau
angeniomba himaya bila shaka ningempa, sisiti juu ya kitu chochote kama
ninavyosita (kuichukua) roho ya mja wangu muumin. Anachukia mauti nami
nachukia kumuumiza.))
(Al-Bukhariy)
WARIDI LA: 4
Fanya mema mengi Allaah Aridhike na wewe na wewe uridhike na uwe tayari kuondoka duniani hali ya kupenda kwenda kuonana naye.
((عن أبي بردة عن أبي موسى
عن النبي صلى الله عليه وآله وسلم قال من أحب لقاء الله أحب الله لقاءه ومن كره لقاء الله كره الله لقاءه))
عن النبي صلى الله عليه وآله وسلم قال من أحب لقاء الله أحب الله لقاءه ومن كره لقاء الله كره الله لقاءه))
((Kutoka kwa Abu Musa kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
kasema: Atakayependa kuonana na Allaah basi Allaah Naye Atapenda
kuonana naye, na atakayechukia kuonana na Allaah, basi Naye Allaah
Atachukia kuonana naye))
(Muslim)
WARDI LA: 5
Ukipendwa na Allaah سبحانه وتعالى basi utapendwa na Jibriyl na wakaazi wa mbinguni na watu wa duniani pia.
((عن أبي هريرة
عن النبي صلى الله عليه وآله وسلم قال إذا أحب الله العبد نادى جبريل إن الله يحب فلانا فأحببه فيحبه جبريل فينادي جبريل في أهل السماء إن الله يحب فلانا فأحبوه فيحبه أهل السماء ثم يوضع له القبول في الأرض))
عن النبي صلى الله عليه وآله وسلم قال إذا أحب الله العبد نادى جبريل إن الله يحب فلانا فأحببه فيحبه جبريل فينادي جبريل في أهل السماء إن الله يحب فلانا فأحبوه فيحبه أهل السماء ثم يوضع له القبول في الأرض))
((Imetoka kwa Abu Hurayrah kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
amesema: Mwenyeezi Mungu Akimpenda mja (wake) Humuita Jibriyl na
Husema: Nampenda fulani kwa hivyo (nawe) mpende. Kisha Jibriyl
humpenda. Kisha Jibriyl huwaita wakaazi wa mbinguni: Hakika Allaah
Anampenda fulani basi na nyinyi mpendeni. Basi hupendwa na wakaazi wa
mbinguni, kisha kupendwa kwake hujengwa duniani))
(Al-Bukhariy)
WARIDI LA: 6
Fanya wema, toa sadaka, jizuie na ghadhabu, wasamehe wenzako wanapokukosea upate daraja ya Muhsiniyn na upendwe na Allaah سبحانه وتعالى
}}الَّذِينَ
يُنفِقُونَ فِي السَّرَّاء وَالضَّرَّاء وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ
وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ وَاللّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ{{
{{Ambao
hutoa wanapo kuwa na wasaa na wanapo kuwa na dhiki, na wanajizuia
ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao
wema}}
(Al-'Imraan 134)
WARDI LA: 7
Penda kusoma Suratul-Ikhlaas upate mapenzi ya Allaah سبحانه وتعالى
((عن أنس أن رجلا قال والله إني لأحب هذه السورة قل هو الله أحد فقال رسول الله صلى الله عليه وآله وسلم حبك إياها أدخلك الجنة
الترمذي وصححه الألباني
Imetoka kwa Anas ambaye alisema: Mtu mmoja alimwambia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم "Mimi naipenda sura hii قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَد akasema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم “Mapenzi yako kwayo yatakuingiza peponi”
At-Tirmidhiy na Imesahihishwa na Albaaniy
(Hapa
tufahamu kuwa Suratu Ikhlaas ni sehemu ya Qur’an, na ni vizuri kuisoma
Qur’an yote na usitosheke na Surah moja au baadhi na ukaacha zingine kwa
kuichukua hadiyth hiyo peke yake bila kutazama na zingine).
WARIDI LA: 8
Mpende Allaah سبحانه وتعالى , Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na Makhalifa wake wote Wanne Abubakar, 'Umar, 'Uthmaan na ‘Aliy رضي الله عنهما upate kuwa nao.
((عن أنس رضي الله عنه
أن رجلا سأل النبي صلى الله عليه وآله وسلم عن الساعة فقال متى الساعة قال وماذا أعددت لها قال لا شيء إلا أني أحب الله ورسوله صلى الله عليه وسلم فقال أنت مع من أحببت قال أنس فما فرحنا بشيء فرحنا بقول النبي صلى الله عليه وسلم أنت مع من أحببت
قال أنس فأنا أحب النبي صلى الله عليه وسلم وأبا بكر وعمر وأرجو أن أكون معهم بحبي إياهم وإن لم أعمل بمثل))
أن رجلا سأل النبي صلى الله عليه وآله وسلم عن الساعة فقال متى الساعة قال وماذا أعددت لها قال لا شيء إلا أني أحب الله ورسوله صلى الله عليه وسلم فقال أنت مع من أحببت قال أنس فما فرحنا بشيء فرحنا بقول النبي صلى الله عليه وسلم أنت مع من أحببت
قال أنس فأنا أحب النبي صلى الله عليه وسلم وأبا بكر وعمر وأرجو أن أكون معهم بحبي إياهم وإن لم أعمل بمثل))
((Imetoka kwa Anas رضي الله عنه ambaye alisema:
Alikuja mtu mmoja akamuuliza Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
kuhusu saa (Qiyaamah) akauliza: Lini Qiyaamah? Akamuulize je, Kwani
umekitayarishia nini? Akasema: sikutayarisha kitu isipokuwa mimi
nampenda Allaah na Mtume wake صلى الله عليه وسلم
Akasema: basi wewe uko pamoja na unayempenda. Anas akasema: Hatukufurahiwa na jambo kama tulivyofurahiwa na usemi huu wa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم "wewe uko pamoja na unayempenda" Akasema Anas: "Basi mimi nampenda Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na Abubakar, na 'Umar na natumai niwe pamoja nao kwa mapenzi yangu juu yao japo kama sikufanya kama walivyofanya wao"))
(Al Bukhariy)
WARIDI LA: 9
Kuwa na Tawakkul katika mambo yako yote, umuweke Allaah سبحانه وتعالى
mbele ya kila jambo, na unapotaka kufanya jambo, kwanza tafuta ushauri
kwa watu wema, kisha swali istikhaara, kisha Tawakkal kwa Allaah سبحانه وتعالى
}}شَاوِرْهُمْ فِي الأَمْرِ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللّهِ إِنَّ اللّهَ يُحِبُّ الْمُتَوَكِّلِينَ{{
{{
Shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee
Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea}}
Al-Imraan: 159
WARIDI LA: 10
Kuwa na tabia njema na watu kama, upole, ukarimu, heshima, ucheshi, adabu nzuri upate kuwa karibu na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم siku ya Qiyaamah.
(( عن أبي جده أنه سمع النبي صلى الله عليه وآله وسلم يقول ألا أخبركم بأحبكم إلي وأقربكم مني مجلسا يوم القيامة فسكت القوم فأعادها مرتين أو ثلاثا قال القوم نعم يا رسول الله قال أحسنكم خلقا))
(احمد)
((Imetoka kwa Abi Jidduh kwamba amemsikia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
akisema: Je, nikujulisheni nani kipenzi kwangu na nani atakayekuwa
karibu yangu siku ya Qiyaama? Wakanyamaza watu wote, akarudia mara
mbili au tatu, wakasema watu: "ndio ewe Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: mwenye tabia njema katika nyinyi))
(Ahmad)
No comments:
Post a Comment