Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, August 31, 2012

ALOZIKWA BUTIAMA


1: NI MINGI SASA MIAKA, TANGU ALIPOONDOKA
    ONDOKA KAMA DHIHAKA, DUNIANI KAFUTIKA
    FUTIKA NA ZAKE TAKA, ZIMEBAKI TWATESEKA
    ALOZIKWA BUTIAMA..............................

2: ALICHOFANYA HAKUNA, TUBAKI KUJIVUNIA
    KUJIVUNIA LA MAANA, URITHI KWA TANZANIA
    TANZANIA TUJE NENA, BABO ALOTUCHIA
    ALOZIKWA BUTIAMA......................

3: AZIMIO ALIUNDA, MALI AKATAIFISHA
   TAIFISHA NA VIWANDA, NA NYUMBA JIMILIKISHA
   JIMILIKISHA NA UKANDA, WA PWANA AKAUFISHA
   ALOZIKWA BUTIAMA.................................

4: ALITUKUZA UDINI, AKAENZI UBAGUZI
   UBAGUZI KWETU PWANI, AKAHUJUMU MAKAZI
   MAKAZI YA VIJIJINI, UJAMAA UKAWINI
   ALOZIKWA BUTIAMA..........................

5: LEO MNAMWITA BABA, SEMENI KWA MKE GANI?
    MKE GANI WA HAIBA, AWE MAMA TAIFANI?
    TAIFANI TUJE SHIBA, ATUOPOE TOPENI?
    ALOZIKWA BUTIAMA.........................

6: LAU LAPIGWA KABURI, NINGELIPIGA LA KWAKE
   LA KWAKE KWA ZAKE SHARI, VIBAYA VITENDO VYAKE
   VYAKE VYA WAZI NA SIRI, ALOFANYA ASIFIKE
   ALOZIKWA BUTIAMA.................................

7: TWAMUOMBA SUBHANA, ATUEPUSHA NA DHAHAMA
    DHAHAMA ZA HUYU BWANA, ALOZIKWA BUTIAMA
    BUTIAMA NANONG'ONA SIJAONA WAKE WEMA
    ALOZIKWA BUTIAMA.......................

8: ALOZIKWA BUTIAMA, SIJAONA WAKE WEMA
    WEMA ULITUAMA, UBAYA UKAUZIMA
    UKAUZIMA DAIMA, USIPATE LA KUSEMA
    ALOZIKWA BUTIAMA............................

No comments:

Post a Comment