Mufti Mkuu waZanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akibadilishana mawazo na
Makamu wa Kwanza waRais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad mara baada
ya kuwasili nyumbani kwakeMbweni kwa ajili ya futari ya pamoja. Katikati
ni Kadhi Mkuu wa Zanzibar SheikhKhamis Haji
Baadhi ya viongoziwa Dini na Serikali pamoja
na wananchi, wakijumuika pamoja katika futariiliyoandaliwa na Makamu wa
Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, hukonyumbani kwake Mbweni.
(picha na Salmin Said, OMKR).
Na Hassan Hamad OMKR
Waislamu nchini wametakiwa kufarijiana ili kutafuta rehema za Mwenyezi Mungu zinazopatikana katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Wito huo umetolewa na Mufti Mkuu wa Zanzibar
Sheikh Saleh Omar Kabi alipokuwa akizungumza na waislamu mbali mbali
katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad huko nyumbani kwake Mbweni.
Amesema kufarijiana sio lazima kuwa na mali
nyingi, bali ni kutoa kitu chochote kwa ajili ya MwenyeziMungu kwa lengo
la kutafuta Rehema na Radhi zake.
“Hata ukitoa kokwa moja ya tende au chupa ya
maji kwa mtu aliyefunga basi inatosha kuwa sadaka yako, nanaamini kila
mmoja wetu anao uwezo huo, bali kitu cha msingi ni kuwa na nia thabiti”,
alifahamisha Sheikh Kabi.
Amesema kitendo cha kufarijiana hasa katika
mwezi huu mtukufu wa Ramadhan kinazidisha umoja,m shikamano na mapenzi
miongoni mwa waislamu, na kuwataka kuendeleza utamaduni huo ambao ni wa
kihistoria kwa Zanzibar.
Amemshukuru Makamu waKwanza wa Rais kwa
kuandaa futari hiyo iliyowakutanisha viongozi mbali mbali wa serikali na
dini wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu na viongozi kadhaa wa dini
akiwemo Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.
Sheikh Kabi ametumia fursa hiyo kuiombea
nchi iendelee kuwa na amani na utulivu, sambamba na kuwaombea viongozi
wa nchi na wazanzibari kwa ujumla, na kuwataka kuepukana na mifarakano
isiyokuwa na maslahi kwa nchi.
“Wananchi sasa tunaishikwa amani baada ya
miaka kadhaa ya mifarakano katika nchi yetu, tunataka amani hii iendelee
na kamwe tusirudi tena huko tulikotoka”, alitanabahisha Sheikh Kabi.
Aidha Sheikh Kabi ametoa wito kwa wazazi na
walezi kuendeleza vitendo vyema ili kuvirithisha vizazi vyao mambo
mazuri ambayo yatawasaidia duniani na akhera.
Kwa upande wake Makamuwa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amewashukuru viongozi hao kwa kuitikia
wito wa kufutari pamoja, na kwamba amepata faraja kubwa kutokana na
mwitiko huo.
Viongozi wengine walioshiriki kwenye futari
hiyo ni pamoja na Katibu Mkuu kiongozi Dkt Abdulhamid Yahya Mzee, Waziri
wa Katiba na Sheiria Mhe. Abubakar Khamis Bakari na mwanasiasa mkongwe
wa Zanzibar Mzee Hassan Nassor Moyo.
No comments:
Post a Comment